Header Ads

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA afuta Posho zisizo na Tija Kwa Watumishi wa Umma

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wialya ya Kigamboni baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wialaya ya Kigamboni  Januari 3, 2016.

..................................

Waziri mkuu wa Tanzania KASSIM MAJALIWA amefuta posho za vitafunwa na zile zisizokuwa kwa mujibu wa sheria katika vikao mbalimbali vya Halmashihauri na kuagiza fedha hizo kutumika katika shughuli za maendeleo.

Waziri mkuu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kigamboni jijiji Dar es salaaam kukagua shughuli za maendeleo akiambatana na watendaji mbalimbali wa serikali.

MAJALIWA amewatahadharishwa wakurugenzi wa manispaa watakaopitisha fedha hizo na kueleza kuwa watachukuliwa hatua kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwajibishwa.

Mapema akizungumza na watumishi wa wilaya mpya ya kigamboni,Waziri mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 waliohamishiwa  Wilaya kigamboni na hadi sasa hawajaripoti katika vituo vyao vya kazi kuripoti mara moja.

Akiwa katika moja ya kiwanda cha kuzalisha maziwa kata ya Kisarawe Two, Waziri MAJALIWA ameeleza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wa viwanda.

Katika ziara hiyo waziri mkuu ametembelea ujenzi wa wodi ya wazazi kata ya Kisarawe Two kisha kumaliza ziara yake katika kiwanda cha uzalishaji maziwa kilichopo kisarawe two na kukagua shughuli za uzalishaji.

No comments

Powered by Blogger.