Header Ads

Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya CCM lafanyika Mkoani Shinyanga


Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini katika mkoa wa Shinyanga kimefanya Kongamano ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM tarehe 05.02.1977.


Kongamano hilo limefanyika leo Katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga,makada wa CCM na vyama vya upinzani na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo wanafunzi wa Shule ya sekondari Buluba na Kom sekondari.

Mada mbalimbali zilitolewa wakati wa kongamano hilo ikiwemo historia ya CCM na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.

Katika kuadhimisha wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM,Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga kitashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya matawi ikiwemo,kupanda miti,kusalimia wagonjwa,watoto yatima,walemavu,kutembelea shule,michezo na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.

Vyama asili vilivyozaa CCM ni Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika  na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar vyote vikiwa ni vyama vya ukombozi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ni "CCM Mpya,Tanzania Mpya".
Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga wakiwa meza kuu.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura,akifuatiwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya,Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid na meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehekea miaka 40 ya CCM watashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo sambamba na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.

Makada wa CCM na wazee wa CCM wakiwa ukumbini.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura alisema lengo la maadhimisho miaka 40 ya CCM ni kujimbusha walipotoka,walipo na wanapoelekea.Kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Rajab Makuburi.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza ukumbini.

Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini.

No comments

Powered by Blogger.