Header Ads

Bodi ya Filamu Tanzania yawakutanisha Wadau Kuandaa Sera ya Taifa ya Filamu.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akitoa mchango wake mbele ya wajumbe wanaoshiriki kikao kazi cha maandalizi ya rasimu ya sera ya filamu nchini. Katikati ni rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba.

 Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu za kitanzania Chiki Mchoma akiwasilisha hoja kama mdau watasnia ya filamu mbele ya wajumbe wa kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu nchini. Wengine kwenye picha kuanzia kuliani Mwnyekiti wa Bodi kuu Sylvester Sengerema, Mwenyekiti wa kikao Vonavyalo Luvanda, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso na rais washirikisho la filamu nchini Simon Mwakifwamba.

Wajumbe mbalimbali wanaoshiriki kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu nchini wakifuatailia kwa makini hoja inayowasilishwa na mmoja wa wajumbe wa kikao hicho(hayupopichani). Kikao hicho kinafanyika mjini Bagamoyo kwenye Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBA).

Wasanii na wadau watasnia ya filamu wanaoshiriki kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu wakifurahia jambo na mwandishi mkongwe wa riwaya na miswada ya filamu AmriBawji(mwenye baraghashia).Kikao kazi hicho kinafanyika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBA).

            .............................................

KILIO cha muda mrefu cha wadau wa sekta ya filamu nchini sasa kinaelekea kupata ufumbuzi wa kudumu baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kuwakutanisha wadau wake kwa ajili ya maandalizi ya sera mahususi itakayotoa mwongozo na kuendeleza sekta hiyo nchini.

Sekta ya filamu nchini imekuwa ikisimamiwa na Sera ya Utamaduni na Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na. 4  ya mwaka 1976 pamoja na kanuni zake.

Kukosekana kwa sera mahususi ya filamu nchini kuliibua changamoto mbalimbali.

 Changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa filamu na michezo mingi ya kuigiza inayotayarishwa chini ya viwango, kutokuwepo kwa mitaji na uwekezaji wa kutosha,sekta ya filamu kutoendeshwa kibiashara, kukosekana kwa mifumo bora ya usambazaji, kutokuwepo kwa weledi na ubunifu wa kutosha, uharamia wa kazi za filamu n.k.

Changamoto zilizoainishwa hapo juu zilibainika baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya tafiti kuhusu hali halisi ya tasnia (situational analysis).

Katika kikao cha kazi cha wadau kilichofanyika tarehe 3 Oktoba, 2016 katika ukumbi wa uwanja wa Taifa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo Nape Nnauye,aliagiza uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania na wizara yake kushirikiana pamoja kuhakikisha sera mahususi ya filamu inapataikana mapema iwezekanavyo.

Sera hiyo mahsusi ya filamu nchini inategemewa kuwa mwarobaini wa changamoto zinzoikabili sekta hiyo kwa muda mrefu sasa.

 Ikumbukwe wadau watasnia ya filamu nchini wamekuwa wa kilalamika kukosa mapato stahili yanayotokana na kazi zao, kushindwa kupata mitaji ya kuwawezesha kuwekeza miundombinu ya kisasa kwenye uzalishaji na mfumo hafifu wa kupambana na uharamia wa kazi zao.

No comments

Powered by Blogger.