Header Ads

Rais Mstaafu ALI HASSAN MWINYI awataka Watanzania kulinda Amani na Utulivu

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani singida Miraji Mtaturu akiwa na Sheikh wa mkoa wa Singida Sheikh Salumu Mahami wakimsindikiza Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi  kufungua msikiti uliojengwa na mbunge mstaafu wa jimbo la Singida magharibi Khalifa  Mohamedi Missanga    mwenye koti jekundu  nyumbani kwake kijiji cha Mnang'ana kata ya Sepuka wilaya Ikungi, ufunguzi huo umefanyika jana  kabla ya  swalatil Jumaa. 

Waumini mbalimbali  waliohudhuria ufunguzi huo  wakimsikiliza mgeni Rasmi Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye viwanja vya msikiti wa Ititi, Sepuka wilayani Ikungi mkoani Singida.

.............................

Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi ametoa rai kwa watanzania kulinda amani na utulivu iliyopo nchini ambayo ni tunu ya Taifa na uhai wa watanzania.

Mzee Mwinyi ametoa rai hiyo wilayani Ikungi mkoani Singida wakati akifungua msikiti uliojengwa na mbunge mstaafu wa jimbo la Singida magharibi Khalifa  Mohamedi Missanga  kijiji kwake Mnang'ana kata ya Sepuka wilaya humo.

Katika salam zake Mzee Mwinyi  amewaasa waislam nchini  kupendana na kuvumiliana na kusisitiza kila mmoja kushika kile anachoamini.

"Ndugu zangu nawaasa tupendane, tuvumiliane,hata kama kuna hitilafu za kimadhehebu zisiwakosanishe,"alisema.

Rais huyo mstaafu aliongeza " hitilafu zipo tu kikubwa ni kushika kile unachoamini na ukitaka kumlingania mwenzako basi iwe kwa lugha laini na yenye heshima lakini kikubwa tulinde amani kwani ndio uhai wetu,"

Msikiti huo uliofunguliwa ulianza kujengwa mwaka 2012 na umekamilika kwa thamani ya milioni 58.

No comments

Powered by Blogger.