Header Ads

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo NSATO MARIJANI awafariji Askari Waliopatwa na Mkasa wa Moto

 
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.



Jengo la ghorofa mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo.


Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao.


Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.


Kamishna Marijani akita pole kwa PC  Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo.


Kamishna Marijani akimfariji  CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea athari iliyotokana na moto huo.


Kamishna Marinaji akimpa pole SGT Hashim baada ya kupoteza vitu vyote vya ndani pamoja na mavazi kufuatia moto ulioteketeza seheumu ya juu ya jengo hilo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuongoza Kamishna Marijani kukagua maeneo mengine  ya jengo hilo ambalo linakumbwa na tukio la moto kwa mara ya pili sasa.


Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi ,Nsato Marijani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kutoa pole kwa asakri waliounguliwa vitu katika jengo hilo.


Waliovalia kiraia ni askari Polisi waliofikwa na janga la kuunguliwa moto vitu vya ndani pamoja na mavazi wakionekana wenye huzuni.


Afisa Mnadhimu daraja la kwanza wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani alipotembelea kambi ya polisi mjini Moshi.


Kamnada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa juu ya tukio la moto katika jengo la makazi ya askari Polisi.


Baadhi ya wanandugu wa familia zilizounguliwa moto wakionekaa wenye huzuni.


Mkuu wa Shule ya Polisi, Kamandanti Matanga Mbushi akizungumza wakati wa kuzifariji familia za askari waliopoteza vitu vyao katika tukio la moto.


Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisni nchini ,IGP Ernest Mangu kwa askari waliopoteza vitu vyao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa katika makazi ya askari Polisi mjini Moshi.


Mmoja wa wageni waalikwa akizungumza wakati akitoa salamu za pole kwa jeshi la polisi. 

No comments

Powered by Blogger.