Header Ads

Naibu Waziri wa Habari ANNASTAZIA WAMBURA aongoza Mazoezi Uwanja wa Samora, IRINGA

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (wa  tatu kutka  kushoto mwenye kikoi shingoni ) akizindua rasmi mazoezi  ya  viungo kwa  mkoa wa Iringa kama agizo la  serikali kila jumamosi ya pili ya  ya mwezi wananchi  wote kushiriki mazoezi ,kushoto kwake ni mbunge wa Kilolo Venance  Mwamoto  na kulia ni mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza. 
 Katibu tawala wa  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayub kulia  akifurahia mazoezi kulia kwake ni mbunge Mwamoto  na mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza.


 Afisa habari  Manispaa ya  Iringa  Sima Bingieki wa  kwanza  kushoto   akishiriki mazoezi  leo uwanja  wa  samora.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wa  pili  kulia  akifurahia  mazoezi na mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Maasenza  wa kwanza  kulia.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wa tatu kushoto na  viongozi mbali mbali wakiongozwa  kufanya mazoezi na Dc Iringa  Richard Kasesela.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura kulia akifanya mazoezi ya  viungo na mbunge  wa  viti maalum mkoa wa Iringa  Ritta Kabati  katika  uwanja  wa  samora  Iringa  leo.
Watumishi  ofisi ya  mkuu wa Mkoa na  RPC Iringa  wakiwa katika mazoezi hayo.
Baadhi  ya  wananchi  wa mji  wa  Iringa  wakiwa  katika mazoezi  leo kutoka  uwanja  wa  samora  kuelekea  ofisi ya RC Iringa.
Hivi ndivyo  wananchi  walivyoshiriki mazoezi  Iringa.
Wananchi  walioshiriki mazoezi  wakiwasili  ofisi ya RC Iringa  wakitokea  Samora.

No comments

Powered by Blogger.