Header Ads

Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA azindua Ufanyaji mazoezi Kimkoa Wilayani Ikungi

Mkuu wa mkoa wa Singida  Rehema Nchimbi akiongoza viongozi na wananchi wa mkoa huo katika uzinduzi wa mazoezi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu la kufanya mazoezi ili kuondoa maradhi yasiyoambukiza na kujenga mwili.
1   Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi katikati akiwa na Mbunge wa viti maalum  Martha Mlata na mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu wakifanya mazoezi ya viungo katika uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akifanya mazoezi  na mbunge wa viti maalum Martha Mlata.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi katikati akiwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu wakiwa na mshindi wa kwanza wa mbio za Mumbai Marathon Alphonce Simbu wakifanya mazoezi baada ya kumpokea.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akicheza muziki baada ya mazoezi na mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ikungi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akionyesha umahiri wake kwenye mazoezi ya viungo.


Mkuu wa wilaya ya Ikungi  Miraji Mtaturu akiruka juu ikiwa ni moja ya mazoezi huku baadhi ya viongozi akiwemo mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi na mbunge wa viti maalum Martha Mlata wakimuangalia.

.................................................
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amezindua mazoezi kimkoa ikiwa ni utekelezaji wa  agizo la makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ili kuondoa maradhi yasiyoambukizwa na  kuimarisha afya za wananchi.

Mbali na uzinduzi huo pia amempokea  shujaa mwanariadha Alphonce Simbu ambaye ni mshindi wa kwanza mbio za Mumbai marathon zilizofanyika mapema mwezi huu huko India.

Akizindua mazoezi hayo leo wilayani Ikungi mkoani humo, Dk. Nchimbi aempongeza Simbu kwa kuwakilisha vizuri katika riadha nje ya  nje na kuwahamasisha vijana kuchamkia fursa hiyo ya riadha kwa kuwa inalipa.

“Singida ni tajiri wa mambo mengi kikubwa tuamue tu,inawezekana kabisa Singida kutoa vipaji zaidi kama tukijipanga,vijana tumieni fursa hii kwani riadha inalipa na inainua uchumi kama  ilivyotokea kwa Simbu,”alisema dokta Nchimbi.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu amemuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa wilaya hiyo imejipanga kuboresha mchezo wa riadha ili kuibua vipaji zaidi vya vijana na kuendeleza sifa ya wilaya na mkoa kwa ujumla katika kutoa wanariadha mahiri watakaoiwakilisha Tanzania kama alivyofanya Simbu.

Ameagiza mazoezi kufanyika jumapili ya pili ya kila mwezi ili kujenga miili yetu na kumpatia Simbu vifaa vya michezo na ahadi ya shilingo milioni moja kwa ajili ya kumsaidia kujiandaa na  mashindano yajayo

Akitoa shukrani kwa mapokezi Simbu ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Mampando,kata ya Ntuntu katika wilaya ya Ikungi amesema mapokezi hayo yamekuwa chachu kwake ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano yajayo.

Akisoma taarifa ya chama cha riadha mkoa katibu wa chama hicho mwalimu  Beno Msanga ameshukuru serikali ya  mkoa na wilaya kwa ushirikiano  wanaoutoa kusaidia mchezo wa riadha na kusema kwa sasa  wana kambi ya wachezaji 15 kujiandaa kwenda mashindano ya mbio za nyika mjini Moshi tarehe 17 february 2017.

Aidha amesema kwa kutambua mchango wa mkuu wa wilaya hiyo Mtaturu chama cha riadha mkoa kimemteua kuwa mlezi wa Chama hicho mkoa wa Singida.

No comments

Powered by Blogger.