Header Ads

JENISTA MHAGAMA aishauri Saccos ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kuwa Wabunifu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akisalimia wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao wa mwaka Uliofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma tarehe 19 Januari, 2017.
...............................

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameshauri uongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu (Makamu Saccos) kuwa na ubunifu katika utendaji ili kuleta manufaa zaidi kwa wanachama wake.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Chama hicho uliofanyika Januari 19, 2017 mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwepo na mikakati madhubuti ya kubuni miradi itakayowezesha chama kuwa na vyanzo vyake vya mapato na kuwa na mikakati ya kuongeza wanachama wapya kwa kuzingatia umuhimu wa chama hicho. 


“Ni muhimu kuwa na mikakati madhubuti ya kubuni miradi, kuongeza wanachama pamoja na kuwa na vitu vya kiupekee na vya kiufanisi vitakavyokisaidia chama kuwa imara katika utendaji wake”, alisema Waziri Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu Januari 19,2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi ada ya uanachama na hisa zake kwa Katibu wa chama Bi. Algensia Ngalapa mara baada ya kuamua kujiunga rasmi na Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Mkutana wao Januari 19, 2017 Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Joseph Muhamba.


No comments

Powered by Blogger.