Header Ads

Wakulima Nchini Watakiwa Kutumia Teknolojia yenye Tija ili Kupata Mazao yenye Ubora

 mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho ya zana za kilimo  katika viwanja  vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani.
  
 Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike   akimuelewesha mkulima jinsi kampuni yao inavyofanya kazi ya kusambaza teknolojia ya umwagiliaji wa Matone.

 Washiriki ambao ni wakulima wakifuatilia kwa makini mada ambazo zilikuwa zikiendelea wakati wa ufunguzi.

   Na Woinde Shizza, Arusha


sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  ufugaji holela , ambao  hupelekea uharibifu wa mazingira,Teknolojia duni pamoja na ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo.



Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho ya zana za kilimo  katika viwanja  vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani  vilivyopo ndani ya jijini Arusha ambapo ni mara ya kwanza kufanyika  .



Alisema kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto za ufugaji holela ambao unasababishwa na wafugaji ,wakulima kutumia teknolojia duni au zazamani katika ukulima  pamoja na wakulima wengi kukosa mitaji ya kubesha miundo mbinu ya kilimo



Alisema kuwa hii inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya sekta hii kutokana na wananchi wengi kutumia kilimo cha kawaida badala yakutumia kilimo cha kisasa ambacho kinaleta tija .



“hapa Tanzania zaidi ya asilimia 75% wanategemea kilimo lakini kati yao n asilimia 1.5 tu ndio wanatumia kilimo  cha kisasa kama kilimo cha umwagiliaji ,kupanda mbegu  bora  pamoja na kilimo cha matone hivyo ni vizuri wakulima wetu kujitaidi kutumia kilimo cha kisasa ili kuweza kufanya kilimo chenye tija ambacho kinamnufaisha yeye mkulima mwenyewe na kuachana na kilimo cha kawaida au naweza sema cha kienyeji”alisema Daqarro.



Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru   amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo ,katika uzalishaji wa Teknolojia ,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.



Aidha alisema kuwa  Seliani wapo  tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi ,ilikuwawezesha wakulima kupata mafunzo na kubadilishana ujuzi  pia iwapo watauwaunganisha itawasaidia  kufahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wasipoteze mazao kama ilivyokuwa kabla ya kupata elimu hiyo ya kilimo.



 mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru   Akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo.

 Washiriki wakifuatilia.

No comments

Powered by Blogger.