Mhandisi MTIGUMWE awaondoa Hofu Watumishi Kuhamia Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo.
Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii
leo amewaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuhusu zoezi la serikali kuhamia
Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za
utumishi wa Umma.
.................................
Mhandisi Mtigumwe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu cha kuhusiana na
uamuzi wa serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi mkoani Dodoma kilichokuwa na
lengo la kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba
na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea mjini Dodoma.
Mtigumwe amebainisha kuwa Awamu ya Kwanza ya uhamisho
utawahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, ambapo katika mchakato huo
watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia tarehe 14 – 15/2/2017 na wengine 47
waliobaki watahamia muda wowote katika kipindi cha kuanzia mwezi Februari hadi kufikia
mwezi Juni.
Mtigumwe amewaeleza watumishi hao kuwa maandalizi
ya ofisi za Wizara ya kilimo zilizopo mjini Dodoma zinaendelea vizuri na tayari
baadhi ya maeneo yamekamilika huku mengine yakiendelea kukamilishwa ili kukidhi
matakwa kwa ajili ya watumishi wote watakapohamia mjini Dodoma.
Uamuzi wa Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na
Uvuvi kuhamia mjini Dodoma ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Serikali yote kuhamia Dodoma
ili kutekeleza uamuzi uliofikiwa tangia miaka ya 70 na Serikali ya Awamu ya
Kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutambua na
kutangaza kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.
Mhandisi Mtigumwe amebainisha hayo hii leo katika
kikao cha pamoja na watumishi wa wizara ya kilimo katika Mkutano huo ulifanyika
Makao Makuu ya Wizara hiyo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment