Header Ads

LAANA TUPU IRINGA " Kaka ambaka Dada yake Amtoa Usichana Wake "

Afisa  maendeleo ya  jamii Manispaa   ya  Iringa  Josephina Mwaipopo  akiwa na mtoto aliyebakwa.
...................................

 Yawezekana ikawa  ni  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa kunyesha  mkoani Iringa tofauti  na  ilivyozoeleka  miaka  mingine  ni  kutokana na laana kama  hizi  baada  ya kikosi  maaalum kinachoongozwa   mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  kwa  kushirikiana na OFM kufanikiwa  kumkamata  kijana Emmanuel Mkiwa  (19) kwa tuhuma  za kumbaka mara kwa mara mdogo wake  wa miaka (4)

Imedaiwa   kuwa kijana  huyo  ambae  ni mwenyeji  wa mtaa  wa Omary  Matrekta kata ya  Mtwivila  katika  Manispaa ya  Iringa alikuwa akiishi nyumba  moja  na babake pamoja na wadogo  zake watatu  wawili  wa  kiume na mmoja  ni  mtoto   huyo  wa  miaka 4  ambaye alitelekezwa  na mamake  mzazi kutokana na mambo ya  kifamilia kati  yake baba  wa  mtoto .
Mashuhuda  wa  tukio   hilo  lililotokea January 16 majira ya  saa 2 usiku walimweleza  mwandishi  wa  OFM  Iringa  kuwa kijana   huyo mara  kwa  mara  alikuwa  akimbaka  mdogo wake  huyo  ambae baba  mmoja  na mama  tofauti kabla  ya  mtoto   huyo kuwaeleza majirani   kuwa kakake  huyo  amekuwa akimkandamiza na  kijiti sehemu  zake  za  siri (Akimbaka)

Kutokana na  maelezo ya  mtoto   huyo ndipo taarifa  za  raia  wema  hao  zilipofikishwa kwa mkuu  wa  wilaya  na OFM na  kuamua  kufika  katika eneo la  tukio na  kufanikiwa  kumkamata kijana   huyo  na baba mzazi  wa  watoto  hao  Shukuru Mkiwa kwa malezi mabaya  ya  watoto.

Akizungumza  baada ya  kukamatwa  kwa  kijana   huyo  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela   pamoja na  kuwashukuru raia wema  kwa  kufikisha taaarifa  ya  kunyanyaswa  kwa mtoto   huyo  bado  alitoa wito kwa  wananchi  wengine  ambao  wanataarifa  za  kunyanyaswa  kwa  mtoto  yeyote  katika  wilaya ya  Iringa  kutoa taarifa  ili  wahusika   wakamatwe  na  kufikishwa  katika  vyombo  vya sheria.

Kasesela  alisema  kuwa uchunguzi   uliofanywa baada ya  vipimo katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa umeonyesha mtoto   huyo kashaondolewa  usichana wake   na  hivyo kulazimika  kulazwa  kwa  matibabu  katika Hospitali   hiyo huku akiahidi kumsaidia mtoto  huyo  kumsomesha .

Alisema  kuwa yawezekana  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa  kunyesha katika  mkoa  wa Iringa  ni  pamoja  na matukio ya  kinyama kama haya ya ubakaji  watoto na  kuwa  hatakubali kuona mbakaji  anaendelea   kuishi  uraiani wilaya ya  Iringa kwani tayari  mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  kupitia  kikao  cha makati ya  ushauri ya  mkoa (RCC)  aliagiza wabakaji wote wasakwe kwa udi na uvumba na yeye ameanza  kutekeleza agizo hilo.

Japo  alisema alishangazwa  na hatua ya baba  mzazi wa  kijana  huyo  kumficha mbakaji ndani na  kudanganya  kuwa  hayupo wakati  kijana  wake  alikuwepo  ndani hivyo  mzazi  huyo  kukamatwa pamoja na kijana  wake yeye kwa  kosa la  kumchifa  mharifu  na kijana wake kwa kosa la ubakaji .

"Hiki  ni  kikosi  kamili  ambacho kitaendelea  kuendesha  misako  mbali mbali kwa kushirikiana na oparesheni  Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hivyo kwa  yeyote  anayejua  wapi  mtoto anafanyiwa  vitendo  vya kikatili piga  simu hii mwandishi wa OFM Iringa 0754 026 299 tutakufikia ulipo na  kuchukua  hatua"



Jeshi la  polisi  mkoa  wa Iringa  kupitia kwa  kamanda wa  polisi  mkoa (RPC) Julius Mjengi limethibitisha  kukamatwa kwa mtuhumiwa   huyo na  kuwa baada ya  upalelezi  atafikishwa mahakamani  huku  likiwataka  wananchi  kuendelea  kufichua  waharifu  zaidi
DC  Richard  kasesela  akiwa amemnyanyua  mtoto  aliyebakwa  akitoka nae kuchukuliwa  vipimo Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa.
 Watuhumiwa  baba  na mwanae  wakiwa   chini ya  ulinzi

No comments

Powered by Blogger.