Header Ads

Waziri wa Habari NAPE NNAUYE azindua Tamasha la Filamu Jijini ARUSHA

 Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .

 Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.
 
 Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mjini Arusha kwenye hotel ya Mt. Meru.

  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha.

  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda  kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite.

 Viongozi wa Arusha wakiwa katika Meza ya Pamoja.

 Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite.

Yvonne Cherry 'Monalisa' pamoja na mama yake, Suzan Lewis 'Natasha' (katikati) wakifuatilia sherehe uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite kwenye hotel ya Mt. Meru.



No comments

Powered by Blogger.