Header Ads

Gari la Abiria latumbukia Baharini Jijini Dar es Salaam waliokuwemo Wahofiwa Kufa Maji

Boti ya mwendo kasi ya JWTZ, ikiwa na wazamiaji imeonekana eneo la mpwani ya magogoni ikiwa kwenye kazi ya kuwatafuta wahanga na gari hilo
................................

GARI aina ya Hiace limetumbukia baharini eneo la Ferry jijini Dar es Salaam mapema leo alfajiri Aprili 20, 2016 na habari zisizo rasmi zinasema watu wawili mwanamke na mwanamme wanahofiwa kufa maji.

Mashuhuda wanasema, wapiga mbizi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ, kikosi cha navy, kwa kushirikiana na wenzao wa jeshi la polisi na kikosi cha zimamoto, wamefanikiwa kuopoa mwili wa mwanamume na kazi ya kutafuta maiti ya mwanamke inaendelea. 

Mashuhuda wanasema, Hiace hiyo ilitumbukia baharini kutoka kwenye kivuko (Ferry) MV-Kigamboni na sababu za kutumbukia kwa gari hilo bado hazijajulikana ingawa mashuhuda wanasemailiteleza. 

Picha zinaonyesha abiria wakishuka nje ya eneola kuegeshea kivuko hicho na hivyo kulazimika kushukia kwenye maji hali inayoonyesha mlango wa kuzuia ulikuwa na hitilafu, Polisi inaendelea na uchunguzi.
Wazamiaji kutoka JWTZ, na Polisi wakiwa kazini.
Waokoaji kutoka kikosi cha Zimamoto nao walikuwepo.

Mwili wa mmoja wa wahanga wa ajali ukiwa umebebwa na waokoaji.

Mwili wa mmoja wa wahanga ukishushwa eneo la kivukoni leo Aprili 20, 2016.

Wazamiaji wa jeshi la Polisi na JWTZ, wakiwa kazini kusaka wahanga wa ajali hiyo.

Kizaa zaa cha abiria kushuka kutoka kwenye pantoni hiyo MV Kigamboni ambayo ilishindwa hata kutia nanga na watu kulazimika kushukia kwenye maji.
Hii ndio hali halisi iliyotokea leo eneo la Ferry.

No comments

Powered by Blogger.