Header Ads

Serikali yapongeza Uanzishwaji wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni TANZANIA


Na: Frank Shija;WHUSM

Serikali yaipongeza Kampuni ya Quality Group ltd kwa hatua yake ya kuanzia Kituo cha Uridhi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) ambapo kupitia kituo hicho bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni zinauzwa ndani na nje ya nchi.

Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho kutaiuza nchi, utamaduni wetu, kazi za sanaa na kuongeza ajira miongoni mwa jamii yetu.

Aidha Profesa Gabriel amesema kuwa Serikali itaendelea kuwa pamoja nao na kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kwamba wanafikia mafanikio na malengo waliyojiwekea katika uwekezaji huo.

Aliongeza kuwa ni vyema sasa Kituo hiko kikafikiria kuanzisha vituo vidogo vidogo katika kanda ili kurahishisha upatikanaji wa bidhaa hizo na kusaidi wasanii walioko pembezoni wapate soko la bidhaa zao kwa Serikali ingependa kuona zaidi wasanii wa ndani wakinufaika na uwepo wa Kituo hicho.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Qaulity Center leo jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi)akitembelea bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni mara baada ya kuzindua rasmi Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifurahia jambo na Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Shadya Karume walipokutaka wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya fimbo maarufu kwa jina la Rungu la Kimasai kutoka kwa Mshauri wa masuala ya bidhaa za sanaa na utamaduni Bibi. Caroline Kessy wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.
..................
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group Limited Bw. Arif Sheikh ameishukuru Serikali kwa kuonyesha ushirikiano kna imekuwa faraja kubwa kwao kwa kiongozi wa ngazi ya juu Serikalini kukubali kuja kuzindua Kituo chao.

Sheikh amesema kuwa kuanzishwa kwa Kituo hicho kumelenga kukuza sanaa na utamaduni wa Mtanzania kwakuwa kinahusika na uuzaji wa bidhaa za sanaa na utamaduni tu, hivyo wasanii wanayo fursa ya kujipatia kipato kwa kukiuzia Kituo kazi zao.

Hata hivyo Sheikh alisema kuwa kutokana na ushauri uliotolewa Kampuni yao ipo tayari kutoa ushirikiano zaidi kwa Serikali pindi watakapohitajika kufanya hivyo ikiwemoi sualaua la kuwajengea uwezo wasanii wa kazi za mikono.


Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzaia ambacho kwa kingereza kinaitwaTanzania Center for Cutural Heritage (TCCH)kipo katika jengo la Quality Center, kinamilikiwa na Kampuni ya Qaulity Group Limited ya jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.