Header Ads

Majambazi yadakwa eneo la Kariakoo baada ya Kuzidiwa Nguvu na Wananchi

Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wakiwa Chini ya Ulinzi mkali wa Polisi eneo la Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam
.....................
Watu wanaosadikiwa majambazi akiwemo “Mburushi” mmoja, wamenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira, kuyaweka “mtu kati” neo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mida hii.

Kama ilivyo kawaida, mamia kwa maelfu ya watu wanaotafuta mahitaji eneo hilo la Kariakoo waliyazingira majambazi hayo baada ya jaribio lao la kupora fedha kushindwa.

Msomaji wa mtandao huu amerusha picha zinazoonyesha majambazi mawili yakiwa hoi bin taaban kwenye eneo la tukio baada ya polisi wenye silaha kuwahi kwenye eneo hilo na kuyaokoa yakiwa tayari yanavuja damu.

Majambazi hayo yakiwa chini ya Ulinzi Mkali wa Polisi, huku wananchi wakiyashangaa katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Umati wa wananchi uliojitokeza kuyashuhudia Majambazi hayo yaliyodakwa na Polisi kwa Kushirikiana na Wafanyabiashara eneo la Kariakoo.

No comments

Powered by Blogger.