Header Ads

Naibu Waziri wa Afya Afanya Mazungumzo na Afisa Miradi Kutoka Shirika la Kimataifa la Nguvu za ATOMIC ( IAEA )

Na Mwanidshi Maalumu

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amekutana na Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile katika mazungumzo yaliyofanyika leo Aprili 14.2016, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Kigwangalla ameomba Tanzania ipatiwe kibali cha kununua mashine mpya ya kutibu saratani (LINAC) Sambamba na sehemu ya msaada iliyoahidiwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw.Yukiko Amano mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Mizengo Kayanda Pinda miaka mitatu iliyopita.

Tanzania tayari imetenga kiasi cha Euro 1.65 Milioni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mchango wake kwa asilimia 50 kama mradi ulivyokuwa awali. Ikumbukwe kuwa, wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA) ndiyo wenye kutoa vibali kwa taasisi ama nchi ambayo itanunua mashine za mionzi hivyo kwa mazungumzo hayo Taasisi hiyo ya Ocean Road ambayo ipo chini ya Wizara ya Afya ipo mbioni kukamilisha upatikanaji wa mashine hizo inazozihitaji.

Mh. Dk. Kigwangalla alisema: “Bahati mbaya sana kutokana na ucheleweshwaji, Bajeti ya msaada huo kutoka IAEA ilipitwa na wakati na kusababisha Tanzania kukosa fursa hiyo. 

Malengo ya Tanzania ni kununua mashine hizo mbili kwa ajili ya kuboresha huduma za tiba ya Mionzi nchini”.

Ujenzi wa jengo kwa ajili ya kufunga mashine hizo mbili umesha kamilika na mashine moja itakamilika mwaka huu na ya pili mwakani ili kuboresha huduma za Saratani nchini.

Katika mazungumzo hayo, Maafisa waandamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Woto walishiriki, akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba, Mratibu wa Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwa watu wazima, Dk. Sara Maongezi pamoja na Kaimu Mkurugenzi taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage.

DSC_1049Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage kabla ya mazungumzo hayo ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dar es Salaam.

DSC_1039Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitolea ufafanuzi moja ya jambo kwa Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile (Hayupo pichani). Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba kutoka Wizara hiyo ya Afya.

DSC_1041Afisa Miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile akielezea jambo katika mazungumzo hayo.

mulongoAfisa Miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile akielezea jambo katika mazungumzo hayo. Wengine ni Naibu Waziri wa Afyaa Dk. Kigwangalla na maafisa waandamizi wa Wizara ya Afya.

DSC_1040Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akisikiliza kwa makini mazungumzo yake na Afisa Miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile (Hayupo pichani) wakati wa mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwa Naibu Waziri. 

(Picha zote na Andrew Chale).

No comments

Powered by Blogger.