Madaktari na Wauguzi wapigwa Msasa Mkoani KILIMANJARO
Mtafiti wa Magonjwa mbalimbali Dkt Ahmed Kalebi akizungumza na madaktari na wauguzi wa Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi wakati wa warsha juu ya matumizi ya maabara ya kisasa iliyofunguliwa mjini Moshi kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali.
Baadhi ya Madaktari na wauguzi katika Hospitari ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Dkt Ahemd Kalebi wakati wa warsha hiyo iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Dkt Kalebi akisisitiza jambo wakati akizungumzia juu ya ufanyaji wa vipimo kwa magonjwa kama saratani na magonjwa mengine ambayo wagonjwa wengi wamekuwa na tabia ya kwenda kutafuta matibabu nje ya nchi.
Baadhi ya Madaktari na Wauguzi katika Hospitari ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi wakiwa katika Warsha hiyo.
Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Josephat Bniface akizungumza jambo katika warsha hiyo ya siku moja iliyoenda sanjari na ufunguzi wa maabara ya kisasa ya Lancet iliyofunguliwa mjini Moshi.
Mtafiti wa magonjwa mbalimbali ,Dkt Ahmed Kalebi akizungumza na wanahabari kuhusiana na mada aliyowasilisha katika warsha hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Post a Comment