Header Ads

ALLY SALUM HAPI ateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya KINONDONI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Ally Salum Hapi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam.

Bw. Ally Salum Hapi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Uteuzi wa Bwana Ally Salum Hapi umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

18 Aprili, 2016

No comments

Powered by Blogger.