Makamu wa Rais SAMIA SULUHU amfuta Machozi MILLEN MAGESE mapambano Dhidi ya ENDOMETRIOSIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu amemfuta machozi Mwanadada, Happiness Millen Magese ambaye ni shujaa wa kipekee kutoka Afrika dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Endometriosis.
Mama Samia amechukua hatua hiyo jioni ya 15 Aprili 2016 wakati wa hafla maalum ya kumkabidhi tuzo.
Katika kilio chake hicho, Millen kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na kumpa kitambaa, mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali ni kwa wanawake wengi hapa Tanzania.
Mama Samia alimwambia kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi lipata ufumbuzi na kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu wake hivyo wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada huyo.
Suluhu alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake, lakini ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo linapewa uzito. Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.
"Nimefurahi kukutana nawe na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika kuhakikisha gonjwa hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila mtanzania kulitambua"alisema.
Akizungumza kwa upande wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuwaelimisha wanawake kuhusu endometriosis.
Alisema Machi 30, mwaka huu Taasisi ya Millen Magese ilikusanya vijana (hususani wa kike) wapatao mia tano kutoka shule za Mugabe, Manzese, Salma Kikwete na Turiani, kuwafundisha, kuwatahadharisha na kuwatanabahi kuhusu Afya, Uenendo, Maisha yao ya kila siku na Changamoto zilizo mbele yao na hususani ikilenga zaidi watoto wa kike ambao wao ndio wahanga wa ugonjwa wa Endometriosis.
Magese alisema watoto hao wakiwafikia hata wenzao 20 tu kila mmoja basi takribani watu elfu kumi watakuwa wamefikiwa.
Tazama tukio hilo:
Mwanadada Jokate Mwegelo akitoa shukrani zake wakati wa tukio hilo. Jakate ni rafiki mkubwa Millen ambapo alimwelezea kuwa, ataendelea kusaidiana na Millen muda wote kwani anatambua harakati za ugonjwa huo ni mkubwa.
Mmoja wa wazazi wa Millen Magese akitoa ushuhuda wa namna wanavyoweza kumsaidia mtoto wao katika mapambano ya ugonjwa huo..
Baadhi ya Madaktari ambao ni wataalam wa kushughulikia tatizo la Endometriosis akiwemo Dkr. Kiiruki wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia na Millen Magese.
Kaka wa Millen Magese akiwa akipata picha pamoja na Mama Samia na marafiki wengine wakiwemo.
Post a Comment