Header Ads

Rais Dkt JOHN MAGUFULI atengua Uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali

Gabriel Nderumaki
...................

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt JOHN MAGUFULI  ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali GABRIEL NDERUMAKI.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ikulu Jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa Rais MAGUFULI ametengua uteuzi huo tangu Machi 18 mwaka huu.

Taarifa iliyothibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi JOHN KIJAZI inamtaja TUMA ABDALLAH kukaimu nafasi hiyo.

Awali TUMA ABDALLAH alikuwa ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN).


No comments

Powered by Blogger.