Header Ads

Wanafunzi Shule ya Msingi Pongwe Wako Hatarini Kwa Sababu ya Ukosefu wa Uzio

Shule hiyo ambayo inapokea watoto wenye matatizo hayo kutokana mikoa mbalimbali Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana uzio huku sehemu kubwa ikipakana na pori jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa ustawi wao kielimu.

Hayo yalibainishwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Waziri Mfaume wakati wa ziara ya Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi aliyoifanya kuangalia changamoto ambazo zinaikabili na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Waziri alisema licha ya kufanya jitihada kubwa za kuanza ujenzi wa
uzio huo eneo la mbele ya shule hiyo lakini mpaka sasa hakuna msaada wowote ambao wamekuwa wakiupata ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linatishia usalama wa watoto hao.

Alisema awali changamoto hiyo ilikuwa eneo la mbele ya shule hiyo na kuona namna ya kulipatia ufumbuzi haraka ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuwavutia wadau kuweza kusaidia lakini suala hilo mpaka sasa limeshindwa kupatiwa tiba.

Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Mtaa wa Pongwe,Hemed Kileo alisema kukosekana kwa uzito kwenye shule hiyo ni jambo la hatari hivyo kuziomba mamlaka husika kuona namna ya kulishughulikia.

Alisema shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1948 ikiwa na darasa la kwanza mpaka la sita ambayo walikuwa wakisoma wakoloni kabla ya mwaka 1957 kubadilishwa matumizi na kuwa shule ya bweni  na baadae ikiwa ni ya mchanganyiko .

Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi akiangalia namna wanavyoandika wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi ya Mchanganyika Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake.
 Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi wa kwanza kushoto akisikiliza kero za wanafunzi hao.

 Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Msingi Mchanganyiko ya Pongwe ya wanafuzi wasiosikia na wenye matatizo ya ngozi (Albino),Waziri Mfaume kulia akimuonyesha diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi maeneo yenye mapori yaliyozunguka shule hiyo ambayo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi hao wakati wa ziara ya diwani huyo.

WATOTO wenye ulemavu wa ngozi na wasioona wanaosoma shule ya msingi ya mchanganyiko ya Pongwe iliyopo Jijini Tanga wapo hatarini kuvamiwa na watu waovu na kuwafanyia vitendo vya kikatili kutokana kukosa uzio na sehemu kubwa kuzungukwa na pori ambalo ni hatari kwa usalama wao.

No comments

Powered by Blogger.