Header Ads

PAC yatoa Miezi 6 Kwa Taasisi na Mashirika Kulipa Madeni

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali( PAC), wakielezwa  na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani( katikati) namna ambavyo kifaa maalum kinachofahamika kama umeme tayari( UMETA) umeme tayari kinavyofanya kazi.
.............................

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) imetoa miezi sita kwa Taasisi  na Mashirika yote kulipa madeni ya ankara wanayodaiwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na endapo watashindwa kufanya hivyo watakatiwa huduma hiyo.

Agizo hilo limetolewa mkoani Mbeya na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC , Livingtone Lusinde wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika kutekeleza Miradi ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati wa Vijijini( REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco.

Lusinde alisema Tanesco imekuwa ikishindwa kutimiza majukumu yake kutokana na kukosa fedha za kutosha kujiendesha na hivyo kuwakosesha wananchi hudumu muhimu ya umeme katika maeneo mbalimbali .

" Tanesco imetapakaa nchi nzima, lakini haiwezi kutoa huduma bora za uhakika kwa wateja wake katika maeneo yote hayo kutokana na miundominu mibovu na kutomfikia mteja kwa wakati kwa vile tu hawana fedha", alisema Lusinde.

Alifafanua kuwa kwa sasa kila Shirika au Taasisi inatakiwa kulipa ankara ya madeni yake moja kwa moja kutoka hazina, hivyo PAC  inaimani kuwa kwa kipindi cha miezi sita hawatarajii tena kusikia malalamiko ya madeni ya ankara kutoka tanesco dhidi ya Taasisi na Mashirika.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiwa katika ziara ya kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.

Wafanyakazi wa Kampuni ya JV State Grid wanaotekeleza Miradi ya Umeme Vijijini katika wakiendelea na kazi ya kujenga miundombinu ya Umeme Vijijini katika kijiji cha Masukulu wilayani Rungwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa( katikati) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, walipomtembelea ofisini kwake, wakati wa ziara ya kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.

No comments

Powered by Blogger.