Header Ads

GAMBIA: Yahya Jammeh atangaza Atang'atuka Madarakani

Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.
Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya "hata tone moja la damu" kumwagika.
Alitoa tangazo hilo baada ya mazungumzo ya saa kadha kati yake na wapatanishi wa Afrika Magharibi.
Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yaliyoafikiwa.
Bw Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Desemba na mrithi wake Adama Barrow tayari ameshaapishwa.
Bw Barrow amekuwa akiishi katika taifa jirani la Senegal kwa siku kadha.
Wanajeshi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika ikiwemo Senegal wametumwa nchini Gambia wakitisha kumtimua Bw Jammeh madarakani.

Adama Barrow, aliapishwa kuwa rais katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal Alhamisi
Uamuzi wa Jammeh kung'atuka aliufanya baada ya kufanya mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania waliofika mjini Banjul Ijumaa kujaribu kumshawishi kuondoka madarakani kwa amani.
"Nimeamua leo, nikiwa na dhamiri njema, kuachia uongozi wa taifa hili kubwa nikiwa na shukrani zisizo na kikomo kwa raia wa Gambia," amesema.
"Namuahidi Allah na taifa lote kwamba masuala masuala ambayo yanatukabili kwa sasa yatatauliwa kwa njia ya amani"
Muda mfupi kabla ya Jammeh kutoa hotuba yake kwenye runinga, Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz alisema kwamba maafikiano yalikuwa yamefikiwa na kwamba Bw Jammeh angeondoka nchini humo.




No comments

Powered by Blogger.