Header Ads

Maadhimisho ya Miaka 10 ya Gazeti la Habari leo yafanyika Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akiwa ameongozana na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz wakielekea katika ukumbi ambako hafla ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo ikifanyika leo 26/01/2017 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wakati wa hafla ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo iliyofanyika leo 26/01/2017 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wakimsikiliza Waziri Nape Nnauye wakati alipokutana nao kwenye Maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo leo 26/01/2017 jijini Dar es Salaam.

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz akiongea na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakati wa hafla ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo iliyofanyika leo 26/01/2017 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye(wa tatu kushoto) pamoja Viongozi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) wakikata keki wakati wa hafla ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo iliyofanyika leo 26/01/2017 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifurahia zawadi ya picha aliyopewa na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bibi. Tuma Abdallah wakati wa hafla ya kutimiza Miaka 10 ya Kampuni hiyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akicharaza gitaa wakati wa hafla ya kutimiza Miaka 10 ya Kampuni hiyo iliyofanyika leo 26/01/2017 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM)

No comments

Powered by Blogger.