Header Ads

Waziri NAPE NNAUYE atembelea Idara ya Habari Maelezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZ0) Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akielezea jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa kwanza kulia) leo jijini Dar es Salaam. Waziri Nape amefanya ziara katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) kwa lengo la kusikiliza changamoto za wafanyakazi wa idara hiyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia saver kwa ajili ya kuhifadhi Picha za matukio mbalimbali alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Afisa Habari Mkuu wa Idara hiyo Bw. John Lukuwi.

Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. John Lukuwi akimuelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye ( aliyekaa) namna Kamera ya kupigia picha za majengo marefu inavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam, Waliosimama wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo (Sehemu ya Habari) Bw. Artemony Tiganya.

No comments

Powered by Blogger.