Header Ads

Serikali yasema Imetenga Fedha ili Kukamilisha Ujenzi wa TERMINAL III

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mara baada ya kukagua jengo jipya la abiria  (Terminal  III) lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNIA, Jijini Dar es salaam.
..................................

Serikali imesema itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha sehemu ya pili ya mradi wa ujenzi wa  Jengo la Abiria la Tatu la abiria (Terminal III) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ili kuboresha huduma za  usafiri wa anga nchini.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi huo sehemu ya kwanza ilifadhiliwa na Benki ya HSBC ya Uingereza hivyo sehemu ya pili Serikali itatoa fedha  ili kukamilisha mradi huo.

”Awamu ya kwanza ya ujenzi huu tulipata mkopo lakini awamu ya pili ya mradi Serikali tumesema hatutachukua mkopo, tutajenga kwa fedha zetu za ndani sababu tuna uzoefu mkubwa wa utekezaji wa miradi kwa kutumia fedha za zetu za ndani'' amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa imarishaji wa viwanja vya ndege nchini unakwenda  sabamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambao mpaka sasa tayari lina ndege mbili aina ya Bombadier Q400.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) akikagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo jipya la Abiria (Tb III) lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNIA, Jijini Dar es salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) Bw. Salim Msangi akisoma taarifa ya utekelezaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) kuhusu Ujenzi wa jengo jipya la abiria (Tb III), lililopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNIA. Jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.