Header Ads

Dkt MAGUFULI afungua Rasmi Awamu ya Kwanza ya Miundombinu ya BRT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa wanahabari mara baada ya kuzindua utoaji huo wa huduma ya usafiri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara baada ya kutoka kukagua moja ya basi linalotumika katika utoaji huduma ya Usafiri wa Haraka (BRT).

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop akimtunza msani Mrisho Mpoto wakati alipokuwa akitumbuiza katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka BRT-Kariakoo huku Rais Dkt. Magufuli akifurahia. 

PICHA NA IKULU

No comments

Powered by Blogger.