Header Ads

Guardiola: Ubingwa EPL ni ndoto

 Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa timu yake kwa sasa inaweza kuondoka katika zile timu zinazowania ubingwa baada ya kupokea kichapo cha 4-0 kutoka kwa Everton.
Kwa sasa City wapo nyuma kwa alama 10 dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 52.
Alipoulizwa kama alama 10 ni nyingi sana alijibu ndio sio rahisi kuzifikia.
Guardiola, mwenye miaka 45, amewaambia wachezaji wake kuungana wakati huu wa kipindi kigumu na kutoangalia msimamo wa ligi mpaka mwisho wa msimu.
''Mwishoni mwa msimu tutajitathimini kiwango chetu,ufundishaji ulikuwaje na wachezaji walikuwaje.
Baada ya hapo tutaamua kwa pamoja.
Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amesema kuwa ana furaha sana kuwa ndani ya Manchester licha ya timu yake kuwa nafasi ya tano.



No comments

Powered by Blogger.