Komredi ABDULRAHMAN KINANA aongoza Mazishi ya Aliyekuwa Katibu wa CCM, Monduli
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo ameongoza mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Jacob Nkomola, yaliyofanyika Mtoni Kijichi, Temeke Dar es Salaam.
Katika mazishi hayo walikuwepo piaa viongozi wengine wa ngazi ya juu wa CCM, wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu. Ngemela Lubinza.
Nkomola ambaye alifariki juzi jijini Dar es Salaam, mwili wake ulitangulia kuagwa nyumbani kwake, Mtoni Kijichi na baadaye kupelekwa katika Kanisa la Kianglikana, Mtoni Kijichi kabla ya kuzikwa katika makaburi yaliyopo Kijichi saa kumi jioni. Kuona mfululizo wa picha tangu kuagwa mwili hadi maziko, tafadhali/>BOFYA HAPA
Post a Comment