Header Ads

Mafunzo ya Wadau wa Filamu Mkoani Mara yahitimishwa Rasmi

Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (katikati) akizungumza hii leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu mkoani humo. Mafunzo hayo yalianza juzi Disemba 14,2016 kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Msoma.
..................................................

Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda, amewahimiza wanatasnia wa filamu mkoani humo kuwa wabunifu katika uzalishaji wa kazi zao ili kupanua soko la filamu ndani na nje ya nchi.

Mapunda ametoa rai hiyo hii leo, wakati akihitimisha mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu mkoani Mara, yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini ili kukuza welezi katika uzalishaji wa kazi bora na zenye maudhui yanaykubalika katika jamii.

"Ubunifu ndio unahitajika hivi sasa, watu wengi wanahitaji ubunifu binafsi na siyo "kucopy" na "kupaste" kazi za wengine". Amesisitiza Mapunda na kuongeza kwamba serikali itatoa ushirikiano wa dhati katika kuboresha tasnia hiyo ya filamu kwani hivi sasa hutoa ajira na kukuza uchumi kwa taifa.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Millao, ameziagiza Bodi za Filamu za mikoa kuhakikisha kwamba zinatimiza wajibu wake ipasavyo ili kuboresha zaidi sekta hiyo.

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisso, amewahimiza wadau wa filamu mkoani Mara wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji walionufaika na mafunzo hayo, kuyatumia vyema ili kukuza soko lao la filamu.

Wanatasnia wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Katibu Tawala mkoani humo, Adoh Mapunda, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia hao. Ameahidi kutoa fulana (Tshirt) 250 kwa ajili ya wanatasnia wa filamu mkoani Mara waliohudhuria mafunzo hayo ambapo zitawasaidia hususani kuwa na sare ya aina moja wakikutana kwa pamoja.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, amesema sekta ya filamu ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wanatasnia wake na taifa kwa ujumla hivyo Bodi za filamu mikoani zihakikishe zinasimamia maendeleo ya tasnia hiyo.

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, amebainisha kwamba wadau wa filamu wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji wamefundishwa vyema mafunzo hayo ili kuzalisha kazi bora.

Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda (wa pili kulia), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, akipokea cheti cha utambuzi.

Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (mwenye suti) na viongozi wengine wakiwa pamoja na washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments

Powered by Blogger.