Header Ads

Mwili wa MPOKI BUKUKU waagwa Dar es Salaam, Kuzikwa Kesho Dodoma

Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwemo wa tasnia ya habari wamejitokeza katika uwanja wa shule ya Tabata, Wilayani Ilala Jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa mpiga picha Mwandamizi wa Magazeti ya The Guardian Limited yanayochapisha magazeti ya Nipashe, The Guardian, Mpoki Bukuku (44) aliyefariki dunia juzi baada ya kupata ajali ya gari.
...........................................

Wadau mbalimbali walipata nafasi ya kutoa salamu zao za rambirambi kwa familia ya marehemu akiwemo waziri wa habari,michezo,sanaa na utamaduni Mh. Nape Nnauye,Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mh. Freeman Mbowe msisitizo mkubwa ukiwa ni wana habari kuyaendeleza mambo mazuri yaliyoachwa na marehemu.

Msemaji wa familia, ambaye ni kaka wa marehemu, Gwamaka Bukuku, amewashukuru watu wote kwa kujitokeza ambapo amewaomba kuendeleza umoja wao kama walivyouonyesha katika msiba huo.

“Mwili wa marehemu baada ya kutoka hapa utasafirishwa kwenda mkoani  Dodoma nyumbani kwa wazazi wake kwa ajili ya mazishi kesho Jumanne Desemba 27,2016 ”amesema.



Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.

Mjane wa marehemu Mpoki Bukuku akisindikizwa kuelekea kwenye eneo la kuaga mwili wa Mumewe.
Mo Blog

No comments

Powered by Blogger.