Header Ads

Kongamano la Vilabu vya Umoja wa Mataifa lafanyika Jijini Tanga


Wanafunzi wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka  vyuo Vikuu na Shule za Sekondari na Msingi kutoka Mikoa mbalimbali nchini wamekutana Tanga kujadili mambo mbali mbali yahusuyo shughuli za Umoja wa Mataifa.

Wanafunzi hao walijadili mambo hayo yakiwemo  Demokrasia na Utawala bora Barani Afrika pamoja na changamoto za Raia katika nchi zenye machafuko.

Pia walijadili uchafuzi wa mazingira kwa nchi zenye viwanda na uharibifu wa mazingira ya bahari kwa baadhi ya viwanda kumwaga sumu baharini.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mlezi wa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransiss Shelutete, amezitaka Serikali nchi za Afrika kuwachukulia hatua kali uchafuzi wa mazingira .




Mwenyekiti wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini Rahim Nassir, akizungumza kwenye kongamano la vilabu vya umoja wa Mataifa lililowashirikisha wanafunzi vyuo vikuu na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
 


Wanachama wa vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kongamano lililohusisha wanafunzi wa vyuoni na Shule za Sekondari na Msingi na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa  Tanga.


Mratibu wa klabu ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransisis Shelutete, akizungumza kwenye kongamano la Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka Mikoa mbalimbali nchini na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga.

No comments

Powered by Blogger.