Header Ads

Mfumo wa Jazia dawa, Vifaa na Vitendanishi Wazinduliwa Mkoani Shinyanga


Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na shirika serikali ya Uswizi leo Jumanne Desemba 13,2016 umezindua Mpango wa Mzabuni teule “Mfumo wa Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi”.
..........................................

Mfumo wa Jazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwa kutumia mzabuni Teule Mmoja ‘Prime Vendor’ ni moja ya mafanikio ya ushirikiano wa sekta binafsi na serikali ukiwa na lengo la kujazia upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya umma vya kutolea huduma za afya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela aliyekuwa mgeni rasmi alisema lengo la mfumo huo ni kuziba pengo linalosababishwa na ukosefu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya afya kutoka Bohari kuu ya dawa.

Alisema kutokana na bohari ya dawa ya serikali kutokidhi mahitaji kila halmashauri hununua dawa kutoka kwa wazabuni wanaowataka matokeo yake bei ya dawa inakuwa kubwa,mlolongo mrefu wa manunuzi na kukosekana kwa njia rahisi ya usimamizi wa mfumo wa ugavi na usambazaji.

"Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya( HPSS Project) unaofadhiliwa na serikali ya Uswizi kupitia shirika lake la Maendeleo (SDC) umeamua kutafuta njia ya kuziba pengo linalosababishwa na ukosefu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi kutoka bohari kuu ya dawa kwa kutumia mfumo wa manunuzi ya nje ya bohari kuu unaohusisha mzabuni mmojatu kwa mkoa mzima,ambaye sasa Bahari Pharmacy Limited",alieleza Msovela.

Naye mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo alisema mkoa wa Shinyanga ni wa pili baada ya Mkoa wa Dodoma kuanza kutekeleza Mpango wa Mzabuni teule huku akisisitiza halmashauri kusimamia matumizi bora ya dawa na wazee kuendelea kupewa kipaumbele.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wakuu wa wilaya,Mkurugenzi wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS),mkurugenzi wa MSD,Mfamasia mkuu wa serikali,mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri,waganga wakuu wa halmashauri na wageni mbalimbali.

Kwa kwanza kushoto ni Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale,katikati ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Desemba 13,2016 wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule “Prime Vendor System” yaani Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi ambapo alisema mfumo huo utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika mkoa wa Shinyanga .Aliongeza kuwa bohari ya dawa ina uwezo wa kuhudumia wateja kwa asilimia 57 pekee katika mkoa wa Shinyanga.

Wa kwanza kulia ni kaimu mkurugenzi wa idara ya Ununuzi na Ugavi ofisi ya rais TAMISEMI Datus Matuma,katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi.Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo.
Wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga wakifuatilia Uzinduzi huo.
Wakuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba,Shinyanga Josephine Matiro na Kahama Fadhili Nkurlu wakiwa ukumbini.

Mbele ni makatibu tawala wa wilaya ya Kishapu, Kahama na Shinyanga.

Wenyeviti wa halmashauri za wilaya katika mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisaini mkataba.

Zoezi la kusaini mkataba linaendelea.

Mwanasheria kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Lightness Tarimo akisaini mkataba huo.

No comments

Powered by Blogger.