Header Ads

Naibu Katibu Mkuu RODRICK MPOGOLO afanya Ukaguzi wa Mali za CCM, Dodoma

 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, Kushoto ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.

 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM.

 Mafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo ukiwa mbele ya jengo hilo la mikutano la CCM.

KUKAGUA MAGARI WHITE HOUSE

 Msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Rajabu Luhwavi, ukiwa umepumzika kwa mda katika jengo la White House la Makao Makuu ya CCM kabla ya kuanza kazi ya kukagua magari, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), akipatiwa maelezo na Fundi wa magari, Ramadhani Mbelwa (kushoto), kuhusu hali ya magari yaliyoharibika, Mpogolo alipokuwa akikagua magari hayo akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amhoji jambo Fundi wa magari ya Chama, Ramadhani Mbelwa (kushoto), alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akionyeshwa gari lililofunguliwa boneti, kupata uthibisho wa gari tatizo la gari, alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimshukuru Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi baada ya kumalizika kazi ya kukagua baadhi ya mali za Chama, mjini Dodoma leo.

KUNZIA SASA HUYU NDIYO BOSS WAKO, SIYO MIMI TENA: Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimtambulisha aliyekuwa Msaidizi wake, Mbwana Kambangwa(kulia), kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo kabla ya kuagana, mwishoni mwa ziara ya Mpogolo kukagua mali za Chama, mjini Dodoma, leo. 

Picha zote na Bashir Nkoromo

No comments

Powered by Blogger.