Header Ads

Hivi ndivyo Mwili wa MPOKI BUKUKU ulivyoagwa Jijini Dar es Salaam

 Baadhi ya Wapiga picha na Wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku baada ya kutolewa heshima za mwisho katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam, tayari kulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi. 

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwaongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam. Mwili wa Mpoki ulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi.

 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku.

 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa akiwa ameshika shada la maua alipokuwa akiingiza kwenye gari lenye jeneza la mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.

 Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo ambaye pia ni Mmiliki wa Blog hii, Richard Mwaikenda akitoa salamu za rambirambi za Chama cha Mabloga Tanzania (TBN) wakati wa kuaga mwili wa mpendwa Mpoki Bukuku.

 Mwakilishi wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo  vya Habari Habari Tanzania (MOAT), Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi.

 Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akitoa salamu za rambirambi.

 Mwakilishi wa Chama cha Wapigapicha za Habar Tanzania (PPAT), Selemani Mpochi akitoa salamu za rambirambi, Mpoki alikuwa mwanachama wa chama hicho.

 ADMIN wa Group la WhatsApp la Tasnia, Thomson Kasenyenda akita salamu za rambirambi na kuahidi group hilo kuwasilisha mchango wao kwa kulipia ada za shule za watoto wa marehemu.

 Mwenyekiti wa Chama cha Bongo Movie, Steven Nyerere akitoa salamu.

 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani Tanzania (TASWA), Juma Pinto akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mpoki Bukuku.

 Benny Kisaka akitoa heshima za mwisho.

 Mhariri Mtendaji wa The Guardian, Mgamba akitoa heshima za mwisho.

 Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Muhidini Issa Michuzi akitoa heshima za mwisho.

 Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mpoki Bukuku.


 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete akitoka kutoa heshima za mwisho.


 Mpigapicha wa The Guardian na Nipashe akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho.

 Mpigapicha wa zamani wa Daily News, Athuman Khamisi akitoa heshima za mwisho.

 Mtoto wa kike wa maraehemu Mpoki Bukuku akimvalisha Rozali wakati wa kuaga mwili wa babake.

 Mjane wa marehemu Lillian  akiubusu mwili wa mumewe.

 Mtoto wa kiume wa marehemu Mpoki Bukuku, Junior akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa babake.


Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Msalato Dodoma kwa mazishi.

No comments

Powered by Blogger.