Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA azindua Mradi wa Uboreshaji Huduma za Umeme Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (katikati) na viongozi wengine kutoka kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (Waziri Mkuu), Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya
usambazaji umeme katika jiji la Dar es
salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016.
.................................................
WAZIRI
Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, amezindua kituo cha udhibiti na
usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es
Salaam, leo Novemba 16, 2016.
Kituo
hicho kipya na cha kisasa, kimejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Norway na
Tanzania, chini ya mpango wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini.
“Serikali
ya awamu ya Tano, iliwaahidi Watanzania, wakati tukiomba kura, ya kwamba,
tutaboresha huduma ya umeme kote nchini, na leo hii ni ushahidi tosha
tunatekeleza kwa vitendo ahadi zetu.” Alisema Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha
Rais wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Akimkaribisha
waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Profesa Sospeter Muhongo amesema,
watanzania wanahitaji umeme tena ulio bora, na sasa kituo hicho ni jawabu la
kuwapatia umeme ulio bora.
“Kati
ya vitu ambavyo sitarajii kuvisikia ni mgao wa umeme, lakini pia bei ya umeme, kuusu
bei tutakaa, pembeni na watu wa TANESCO kulizungumzia hili. “ Alitoa hakikisho
Waziri Muhongo.
Kwa
upande wake, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen, alisema,
teknolojia iliyotumika kwenye mitambo ya kituo hicho ni ya kisasa ijulikanayo
kama Distribution SCADA System, na
inauwezo wa kutambua hitilafu ya umeme kwa haraka na hivyo kurahisisha
kurekebisha hitilafu hiyo kwa wakati.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema, Mradi wa
uboreshaji huduma za umeme jijini Dar es Salaam ulibuniwa kwa lengo la
kuboresha miundombinu ya umeme katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko
kubwa la mahitaji ya umeme katika sekta za kiuchumi hususan katika maeneo ya
katikati ya jiji, Kariakoo, Ilala na maeneo ya wilaya ya Kinondoni.
Alisema,
utekelezaji wa mradi huu umehusisha ujenzi wa kituo cha kupoza nguvu za umeme
chenye ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV cha City Centre, ujenzi wa mfumo wa
njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmission Line) na
kwa kutumia minara (Overhead Line) ya msongo wa wa kilovolti 132 kutoka kituo cha
Ilala hadi kituo cha City Centre umbali wa Kilomita 3.4, vile vile ujenzi wa
mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission
Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita
6.67.
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu, kituo hiki ambacho kinajulikana kitaalamu kama Distribution SCADA System
kitawezaesha watoa huduma wetu kufuatilia kwa haraka zaidi pale matatizo ya
umeme yanapojitokeza kwa kutumia mifumo ya ksiasa ya kompyuta.” Alifafanua
Mhandisi Mramba na kuongeza.
“Nia
hasa ni kujenga vituo vingine kama hiki kwa kuanza na miji mingine mikubwa ya
Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma.” Alisema.
Waziri Mkuu na wageni wengine wakitembelea chumba cha mitambo yaudhibiti na
usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme Distribution SCADA System.
Waziri Mkuu akitembeela moja ya mitambo inayopatikana kwenye kituo chicho (Server).
Mtaalam wa mitambo, wa shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Bi, Mwajua Turkey, kushoto, akimpatia maelezo waziri mkuu wakati akitembelea kituo hicho muda mfupi kabla ya kukizindua rasmi.
Waziri Mkuu akitoa hotuba yake.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akitoa hotuba yake.
Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen.
Waziri Mkuu, akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, (wapili kushoto), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo, (kushoto) na Waziri Kai(kulia), wakishangilia baada ya uzinduzi.
Post a Comment