UNESCO - TANZANIA yawajenge Uwezo Maafisa Kutoka Wizara ya Habari
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigueas, (kulia), akiendesha semina ya mafunzo ya siku tatu kujenga uwezo kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, makao makuu ya UNESCO, Oysterbay jijini Dares Salaam, leo Novemba 30, 2016. Kushoto ni Mwanasheria wa Wizara, Bw.Evordy Kyando.
Na Khalfan Said
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni , (UNESCO), limeendesha
mafunzo ya siku tatu kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, ili kuwajengea uwezo wa kutekeelza mpango mkakati wa wizara hiyo kwa
mwaka wa fedha 2016/2017.
Mafunzo
hayo yaliyoanza leo Novemba 30, 2016, na kuendeshwa na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO,
nchini, Bi. Zulmira Rodrigues yanafanyika kwenye ofisi za shirika hilo,
Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Tumekusanyika
hapa kwa mara ya kwanza kuisaidia wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ili kuboresha uwezo wawafanyakazi wake, wafanyakzi kutoka idara tofauti tunao
hapa, wapo kutoka idara ya Habari, Utamaduni, michezo pamoja na idara za
kiusaidizi kama vile fedha, sheria, ICT na kadhalika.” Alianza kwa kusema Mkuu
huyo wa UNESCO.
Alisema,
Mpango unaweza kusaidia kufanya tathmini na marekebisho kwa mahitaji ya wizara
au taasisi yoyote ile na kwa kuzingatia hilo, Shirika hilo limeona upo
umuhimowa kuwajengea uwezowatendaji katika wizara hiyo ili kutekeleza vema
mpango mkakati wa wizara. “Kama huna mpango wowote ule uliouweka, utajikuta
unatumia nguvu nyingi na kuishia patupu bila mafanikio yoyote yale.” Alisema.
Alisema,
wafanyakazi katika taasisi yoyote ile ni wajibu kushirikiana ili kuwa na lengo
moja kufikia malengo mahsusi yaliyopangwa na Wizara au taasisi. “Kabla ya
kuweka mpango wowote ni lazima kufanyike utafiti wa hali halisi ya jambo
linalotaka kushughulikiwa.” Alifafanua Bi. Zulmira.
Washiriki
walianza kujifunza mambo mbalimbali ama vile, namna ya kutambua tatizo la
msingi, uwezo, udhaifu, fursa na tishio mambo yote hayo yanayojulikana
kitaalamu kama (SWOT Analysis), ndiyo yatakayotoa picha halisi ya namna ya
kupanga mkakati na namna ya kuutekeleza mkakati huo.
Aidha
washiriki wa warsha hiyo wamefurashiswa na mafunzo hayo kwani yatasaidia
kuwajengea uwezo wa kutekeelza kikamilifu malengo ya kiofisi na binafsi.
“Mafunzo
haya yatanisaidia sana katika kutekeleza malengo yaliyopangwa kwani nimejifunza
njia mbalimbali za kimkakati katika kutekeleza malengo yaliyopo.” Amesema
mshiriki Lorietha Lawrence, afisa habariwizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kupitia
mafunzo haya, ninahakika yatasaidia kutekelza majukumu yangu ya kila siku, na
nitakachojifunza nitashirikiana na wenzangu kwenye kitengo chetu katika
kutekelezaipasavyo majukumu yetu.” Alisema Afisa mwingine wa habari, Lilian.
Baadhi ya washiriki.....
Mshiriki kutoka idara ya utamaduni, Sefania Molela, akizungumza.
Mshiriki kutoka idara ya Habari akizungumza.
Post a Comment