Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake Novemba 25, 2016
Ukatili dhidi ya wanawake ni uvunjaji mkubwa wa haki za msingi za binadamu na tishio kwa mamilioni ya wasichana na wanawake duniani kote.
Takribani mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu duniani amekuwa akipigwa, kulazimishwa kufanya ngono, au kunyanyaswa vinginevyo katika maisha yake.
Jamii nzima imeathiriwa na ukatili ambao unaweza kuwa wa kimwili, kingono (unyanyasaji, kulazimishwa au kubaguliwa) na kisaikolojia (kunyanyaswa kwa maneno au kwa hisia, kama vile kuonewa au kutengwa).
Katika siku hii ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, UNESCO inaangazia mabadiliko ya tabia nchi na uhaba wa rasilimali kama sababu za kuchochea ukatili dhidi ya wanawake – nyumbani, mitaani, wakati wa majanga asilia yanayosababishwa na tabia nchi.
Mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha tishio - yanaweza kuongeza uhamaji na kukosa makazi kwa watu na kuchangia katika kutokuzalishwa kwa mazao au mafuriko, kuongeza msukumo nyumbani na katika utafutaji wa riziki.
Utafiti unaonyesha kwamba wanawake wanawajibika kwa asilimia 65 ya uzalishaji wa chakula katika kaya huko Asia, kwa asilimia 75 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa asilimia 45 huko Amerika ya Kusini.
Mara nyingi, ni wajibu wa kiutamaduni wa wanawake unaowaweka katika hatari kubwa dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi – na kwa hiyo kujikuta wakiwa katika mazingira yenye uwezekano wa kufanyiwa ukatili wanavyotembea maili nyingi kila siku kutafuta chakula, maji na kuni au baada ya kukosa makazi au kupata umasikini kutokana na majanga.
Kukosa njia za kujitafutia riziki na umasikini kunaweza pia kusababisha ukatili nyumbani kutokana na msukumo wa kiuchumi, pamoja na kuendelea kwa muda mrefu kwa mienendo ya ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni.
UNESCO inashiriki kikamilifu katika kuimarisha ujasiri wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi, ujumuishaji wa mkabala wa kijinsia katika utendaji wake wote.
Kwa kutumia ushirikiano na mipango ya kibunifu, UNESCO inaendeleza fikra inayodai kuwa wanawake na wasichana ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hasa, kwa mfano, mipango ya kusimamia maji na utayari wa kukabiliana na majanga.
Tunafahamu kwamba uzalishaji wa gesi ukaa unaiathiri sayari ya dunia. Tunapaswa pia tutambue kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri maisha ya wasichana na wanawake duniani kote.
Tunapokuwa tupo tayari kuanza kutekeleza Mkataba wa Tabia Nchi wa Paris na kujiandaa kwa ajili ya mafanikio ya COP22 huko Marrekech, tusiisahau nusu ya idadi ya watu wetu na uwezo wao mkubwa wanaouwakilisha.
Wanawake lazima wawe katika kiini cha utatuzi wote wa mabadiliko ya tabia nchi.
Post a Comment