Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa matamasha ya Mtikisiko yanayolenga kunyanyua sekta ya muziki yatakayofanyika katika mikoa katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya kwa uratibu wa radio ya Ebony FM.
....................................................
Kampuni inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania
leo imesaini rasmi uzinduzi wa tamasha
la mwaka la Mtikisiko kwa kushirikiana
na kituo cha redio cha Ebony FM ambacho kina wasikilizaji wengi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Mtiririko
wa matamasha hayo ya mwaka unatarajiwa kuanza Novemba 19 hadi 26 katika mikoa ya Njombe na Mbeya kwa pamoja ambapo onesho la fainali litafanyika Desemba 10, 2016 mkoani Iringa.
Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo mkoani Iringa,
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini
Jackson Kiswaga alisema, “Tigo kila mara
inakuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha kwamba vipaji vinavyoibukia
katika sekta ya muziki vinapewa jukwaa
la kuonesha vipaji vyao na wasanii maarufu wanaweza kuunganishwa na mashabiki
wao.
Tamasha la Mtikisiko
linakuja baada ya kumalizika kwa Tamasha la Tigo Fiesta 2016 hivi
karibuni ambalo Tigo ilikuwa mdhamini
mkuu. Kiswaga aliwaaambia waandishi wa habari kwamba mashabiki watarajie ubora
ule ule wa burudani waliouzoea
wakati wa tamasha la Fiesta.
Kushiriki kwa Tigo kutakwenda sambamba na kuhakikisha
wateja wa Tigo na wale ambao sio wateja
wanafahamu na kuzielewa huduma za
Tigo wakati wa tamasha.
“Katika kukuza uzoefu
wa mteja na mtumiaji wakati wa tamasha,
tunatarajia wateja wetu kutumia vilivyo
kuanzishwa kwa huduma ya 4G LTE, Tiogo Pesa
na bidhaa na huduma nyingine zinazotolewa,” alisema Kiswaga.
Kiswaga alitangaza kuwa washiriki wa tamasha hilo kwa mwaka
huu watakuwa na nafasi ya kuchagua njia ya kupata tiketi zao kupitia Tigo Pesa bila gharama ya ziada.
Kwa mujibu wa
mkurugenzi huyo washiriki wote wa
tamasha ambao watanunua tiketi zao kupitia Tigo Pesa watafurahia faida kwa kupata [punguzo la
asilimia kumi kwa kila tiketi
itakayonunuliwa
Kiswaga alifafanua, “Kununua tiketi kupitia Tigo Pesa,
wateja kutoka mtandao wowote watapiga
namba ya Mfumo wa Kifedha wa Simu (mfano *150*01# kwa Tigo), halafu chagua,
“tuma pesa”, ikifuatiwa na chagua, “Mitandao Mingine” halafu chagua, “Tigo
Pesa” na mwisho ingiza namba 0674444444.
Kwa upande wake
mratibu wa Tamasha la Mtikisiko 2016, Austine Nyondo alisema, “Ninapenda
kuchukua nafasi hii kuwaashukuru Tigo wakiwa ni wadhamini wakuu wa tamasha
hili; mashabiki wetuwatarajie kupata burudani kutoka kwa wasanii maarufu katika sekta ya
muziki.”
Aliarifu kuwa wakati wa tukio hilo watasambaza vipeperushi kwa vijana ambavyo vitakuwa na ujumbe unaohusu Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutokana na
sababu kwamba mikoa ya kusini
inachukuliwa kuwa ni “ukanda
ulioathiriwa” na janga hilo.
Tamasha maarufu la Mtikisiko ambalo awali lilijulikana
“Together Time” lilibadilishwa jina
mwaka 2008 lilianza mwaka 2007 na
limeendelea kukua katika kipindi chote
cha miaka hiyo na kupata umaarufu kama tamasha la burudani la mwisho wa
mwaka katika mikoa ya kusini.
|
Post a Comment