Header Ads

Rais Dkt MAGUFULI awatunuku Kamisheni Maafisa Wapya 194 wa JWTZ


Bendi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) likiingia uwanjani wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki kuimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa zawadi kwa mmoja ya wanafunzi waliofanya vizuri katika kozi ya mafunzo wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku kamisheni Maafisa wapya 194 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ).

Maafisa wapya 194 wakila kiapo cha uadilifu baada ya kutunukiwa kamisheni katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi (TMA) Meja Generali Paul Massao(Kulia) kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi (TMA) Meja Generali Paul Massao akitoa taarifa fupi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya mafunzo kwa maafisa wa jeshi ambapo alisema kozi ya mafunzo hiyo ya mafunzo ilianza na wanafunzi 222 kabla ya kuchujwa na kubaki 194 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutofikia viwango.

Picha na Hassan Silayo

No comments

Powered by Blogger.