( MAKALA ) Hifadhi ya Taifa ya KATAVI na Vivutio vyake vya Asili
Mmoja wa Simba akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Baadhi ya Mamba wakiwa wamepumzika katika hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali.
Simba akiwa na mzoga wa Kiboko.
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Na Walter Mguluchuma
Hifadhi ya Taifa ya Katavi inapatikana kusini Magharibi mwa Tanzania karibu na Ziwa Tanganyika katika Wilaya za Mpanda ,Tanganyika na Mlele Mkoa wa Katavi inapatikana katika latitude 6.63.7.34 kusini na na longitude 3.74.31.84 Mashariki.
Hifadhi hii ilitangazwa kuwa Hifadhi ya Taifa mwaka 1974 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 2253 iliongezwa ukubwa mwaka 1996 na kufikia ukubwa wa kilometa za mraba 4471 na kuifanya kuwa Hifadhi ya tatu kwa ukubwa Tanzania baada ya Ruaha na Serengeti .
Ilipata jina lake kutokana na mzimu wa kabila la Wabende aliyejulikana kwa jina la Katabi ambapo mpaka leo watu mbalimbali wamekuwa wakifika ndani ya Hifadhi ya Katavi na kwenda kwenye mti ulioko kwenye Ziwa Katavi wakiamini kuwa mzimu Katabi alikuwa akiishi hapo zamani kabla ya kuwepo Hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Jina la Hifadhi hii lilijulikana kama Katabi kutokana na imani ya jamii hizo kwa mzimu Katabi inaaminika kwamba mzimu Katabi una uwezo wa kufanya miujiza ikiwemo kufanya mvua inyeshe , kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali .
Hifadhi hii inafikika mwaka mzima kwa kupitia Mikoa ya Dares,salaam,Mwanza , Kigoma Arusha hadi Mpanda kupitia Tabora kwa kutumia usafiri wa ndege za kukodi Chartered planes au kwa njia ya barabara kwa kupitia Mbeya na Sumbawanga pia kwa kutumia usafiri wa Treni kutokea Tabora .
Katavi 'National Park' inawanyama wengi na adimu na wakubwa kuliko wanyama wanaopatikana kwenye Hifadhi nyingine hapa Nchini kutoka na hari ya uoto wa asili uliopo kwenye Hifadhi hii ambayo kwa sasa imeanza kupata watalii tofauti na hapo awali .
Mbali ya kuwepo kwa wanyama wengi madhari yake ni pana kuanzia uwanda tambarare wa nyasi katika mkondo wa bonde la ufa hadi kwenye miteremko mikali ambayo ni matawi mawili sambamba na bonde la ufa la Mashariki maarufu kama bonde la ufa la Rukwa .
Uoto uliopo unavutia unavutia sana kuanzia kuanzia Misitu iliyofunga mpaka misitu ya wazi ,vichaka uwanda wa nyasi maziwa ya msimu ya Chada na Katavi mabwawa na uoto kando ya mito .
Wakati wa kipindi cha mvua kuna aina nyingi za maua aina ya 'species' mbalimbali za miti na majani aina za 'species' 226 za miti zimeisha tambuliwa zikiwemo aina tatu zenye mvuto wa kisayansi .
Uhai wa Hifadhi ya Katavi unategemea mto Katuma ambao humwaga maji yake ziwa Katavi upande wa kaskazini ,Ziwa Chada na mbuga yenye eneo la kilometa za mraba 425 ambayo hutuamisha maji Floodplain katikati ya Hifadhi ziwa Chada hupokea pia maji kutoka mto Kapapa ambao mkondo wake hutokea Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Katavi .
Kuna aina mbalimbali za wanyama pori ,idadi kubwa ya vipepeo na ndege wa aina mbalimbali katika Hifadhi ya Katavi ni kivutio vikubwa kwa wageni idadi ya watalii na shughuli za maendeleo ndani ya Hifadhi bado ni ndogo hivyo kufanya mazingira kuwa asilia zaidi .
Baadhi ya wanyama wanaopatikana kwenye Hifadhi ya Katavi ni makundi makubwa ya Tembo , Nyati, Simba , Pundamilia , Mbwa mwitu , kongoni Swala pala , Nyemela na wanyama wengineo .
Pia kwenye eneo la mto Stalike na Iku utakuta kuna makundi makubwa sana ya viboko na mamba ambapo kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara na kufanya eneo hilo kuwa kivutio kikubwa kwa watalii.
Upande wa Hotel hifadhi hiyo inayo hotel nzuri za kufikia wagani ndani ya Hifadhi iiingawa bado ni chache pia hotel nyingine zinapatikana katika Kijiji cha Stalike ambacho kipo jirani na Hifadhi na pia katika Mji wa Mpanda makao makuu ya Mkoa wa Katavi uliopo umbali wa kilometa 40 kutoka Hifadhi ya Katavi .
Hivi karibuni kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Elias Manase aliwaambia wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wa Mkoa wa Katavi kwamba Hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali .
Baadhi ya changamoto hizo ni ujangili wa wanyama hasa Tembo ambao unasababishwa na kuwepo kwa kambi za wakimbizi za Mishamo na Katumba ambazo wanaishi Raia wa Burundi na Kongo .
Ilidai kuwa watu wanao ishi kwenye makazi hayo wamekuwa wakiingiza silaha za kivita na kuziingiza nchini kisha wamekuwa wakifanya ujangili wa kuuwa Tembo na kisha wanachukua meno ya Tembo na kuyasafirisha kwenye soko la nchi jirani.
Changamoto nyinginei ni uhaba wa miundo mbinu ndani ya Hifadhi kwani bado haiku mizuri sana ingawa barabara zake zinapitika karibu mwaka mzima .
Manase alitowa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea Hifadhi za Taifa kwani gharama ya kutembelea Hifadhi za Taifa ni ndogo kuliko gharama ya mtu anayoitumia kwenye Bar kunywa pombe .
Askari wa Hifadhi ya Katavi Joseph Mhina aliielezea Hifadhi ya Katavi kuwa ni hifadhi ambayo ipo tofauti kabisa na Hifadhi nyingine kwani watalii wanaotembelea Hifadhi hiyo huwa wanawaona wanyama kiurahisi kabisa kwani watalii huwa ni wachache hivyo huwa hakuna kugombania kuwaona wanyama kama Hifadhi nyingine .
Post a Comment