PAUL MAKONDA akutana na Ujenzi Hewa wa Barabara Wilaya ya Ubungo
PAUL MAKONDA |
Wakati imezoeleka kusikia kuwepo kwa wafanyakazi hewa leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paull Makonda ameshangaa baada ya kubaini kuwepo barabara hewa ambayo ujenzi wake umegharimu mamilioni ya fedha katika kata ya Msigani, wilayani Ubungo.
Makonda alielezwa kuwa ipo barabara ambayo inajengwa kwa usimamizi wa mtendaji wa Kata hiyo, lakini cha kushangaza barabara hiyo haipo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Barabara (TANROADS) wala Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambayo ndiyo inayosimamia kwa kuwa bado Wilaya ya Ubungo haijawa na Halmashauri.
Ilielezwa katika mkutano uliofanyika kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Temboni Kata ya Msigani, kwamba barabara hiyo ni inayotoka Msigani kwenda Kinyerezi.
Kufuatia malalamiko kuhusu barabara hiyo, Makonda aliamuru Polisi kumsaka Mwenyekiti huyo wa mtaa na kumhoji pamoja na wale wote alioshirikiana nao katika kadhia hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole (kulia), kuhusu mradi wa maji wa Kata ya Temboni Kata ya Msigani, alipokagua mradi huo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi wa papo hapo au wa baadaye katika wilaya hiyo.
Makonda akitazama tanki la maji la mradi huo.
Makonda akionyeshwa bomba la maji lililopo karibu na tangi la maji la mradi huo.
Baadhi ya wananchi wakimweleza Makonda kero zao kwa njia ya bango alipokuwa kwenye mkutano kwenye Ofisi ya Mtendaji mtaa wa Temboni, Kata ya Msigani.
Mkuu wa wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Paul Makonda kuzungumza na wananchi.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makonda kwenye mkutano huo.
Mkazi wa mtaa wa Temboni, Moreen Gomba akitiririka kueleza kero wakati wa mkutano huo uliofanyika mbele ya Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Temboni, Kata ya Msigani wilayani Ubungo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisikiliza kwa makini wakati wananchi wa Kata ya Msigani wakieleza kero zao kwenye mkutano aliofanya kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Temboni, leo, Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole.
Makonda akimhoji maswali Mtendaji wa Mtaa wa Temboni, Ramadhani Dilolo (kushoto), kuhusu kero zilizoelekezwa kwake na wananchi wakati wa mkutano huo.
UZINDUZI MRADI WA MAJI KATIKA SHULE YA SEKONDARI GOBA MPAKANI
Maelezo mafupi ya mradi huo.
Makonda akizungumza kabla ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa na mfadhili katika Shule ya Sekondari Goba Mpakani.
Makonda akizindua mradi wa maji katika shule ya sekondari ya Goba Mpakani, akiwa katika ziara hiyo, leo.
Makonda akimpongeza mfadhili wa mradi huo wa maji, Husein Afif, Kushoto ni Polepole.
Makonda akimpongeza Polepole baada ya kuzindua mradi huo wa maji. Baada ya kuzindua mradi huo Makonda aliahidi kugharamia ujenzi wa visima vinane katika Kata ya Goba.
MTAA WA MATOSA, KATA YA GOBA
Kijana akiwa ameshikiliza bango kufikisha kero kwa Makonda kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Matosa kata ya Goba.
Mkazi wa mtaa wa Matosa akifurahia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanywa na Makonda katika mtaa huo leo.
Makonda akimsilikiza kwa makini Polepole wakati akimshauri jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika mtaa wa Matosa.
Wanafunzi wakitumbuiza kwa kwaya wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Matosa.
Makonda akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika katika mtaa huo.
Mwananchi wa mtaa wa Matosa akieleza kero kwa Makonda wakati wa mkutano huo.
UKAGUZI KITUO CHA UTABIBU CHUO KIKUU CHA SAYANSI YA TIBA CHA MUHIMBILI (MUHAS) KAMPASI YA MULONGANZILA WILAYANI UBUNGO
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo alipokagua eneo la hifadhi ya umeme, kwenye kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo alipokagua eneo la kuzalisha umeme, kwenye kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo alipokagua eneo la kutoa umeme wa dharua, umeme unapokatika kwenye mitambo ya kuzalisha umeme, kwenye kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiendeleakupata maelezo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua kwa kina eneo la mitambo ya kuzalisha umeme, kwenye kituo hicho.
Makonda akitazama sehemu ya kunasa na kuhidhadhi kumbukumbu za matukio yanayofanyika katika jengo la Kituo hicho.
Makonda akitazama kitanda na vifaa maalum katika chumba cha upasuaji.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha MUHAS,Profesa Elisias Lyamuya akitoa maelezo mbele ya Makonda kuhusu utendaji na changamoto za Kituo hicho Kampasi ya MUHAS ya Mlonganzila.
Makonda akitoa nasaha zake kabla ya kuondoka kwenye kituo hicho.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa MUHASAmos Nnko akimsindikiza makonda wakati akiondoka.
Post a Comment