Wanatasnia ya Filamu Mkoani Geita Wapewa Mtihani wa Kuandaa Tamasha la Filamu
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.
Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (wa pili kushoto).
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.
Baadhi ya wanatasnia ya Filamu mkoani Geita waliohudhuria kikao baina yao na Bodi ya Filamu mkoani humo, wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso, ambapo amewasisitiza kuungana pamoja na kutengeneza filamu moja iliyo bora kwa ajili ya kuwatambulisha kwenye soko la filamu na pia kuutambulisha mkoa wa Geita badala ya kuwa na filamu nyingi zisizo na ubora.
Kutoka kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye.
Wanaofuata ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fessoo, Mwakilishi wa balozi wa Tanzania nchini Denmark, Dotto Kahindi pamoja na Mratibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), Robert Manondolo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akisisitiza wasanii mkoani Geita kushikamana na kushirikiana na viongozi wao pamoja na Serikali na kuandaa Tamasha la Filamu kwa kuwa fursa hiyo wanayo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita amesema viongozi wa serikali mkoani Geita wakiwemo Maafisa Utamaduni wako tayari kutoa ushirikiano wao ili kuboresha tasnia ya filamu mkoani humo.
Amewapa chachu wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuungana pamoja na kutengeneza kazi bora kwani sanaa hiyo inaweza kubadilisha maisha yao na kuwa mabilionea ikiwa watafanya kazi bora.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael, amebainisha kwamba chama hicho kimeweka mikakati ya kuboresha soko la filamu mkoani Geita huku matamanio yao ni kuwa na Tamasha la Filamu ili fursa kwa wasanii kuonesha kazi zao.
Mmoja wa wanatasnia ya filamu mkoani Geita akisoma risala kwa niaba ya wasanii wengine ambapo amebainisha kwamba wanasanii wa filamu mkoani Geita wanahitaji kupewa mafunzo zaidi namna ya kuboresha kazi zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi zao hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao.
Na George Binagi
Wanatasinia ya Filamu mkoani Geita wamepewa mtihami ambao hata hivyo ni mwepesi ikiwa watakuwa na dhamira ya dhati ya kuikuza tasnia hiyo.
Mtihani huo umetolewa hii leo na Waziri wa Afya Zanziar, Mahmood Kombo, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye kikao baina ya wasanii wa filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu nchini.
Mtihani wenyewe ni wanatasnia hao kwa kushirikiana na chama cha Waigizaji mkoa wa Geita, kuandaa Tamasha la Filamu mkoani Geita ambalo litasaidia kuinua tasnia hiyo mkoani humo, Kanda ya Ziwa na hata nchini kwa ujumla.
"Mkitayarisha Tamasha lenu, mimi mwakani nitakuja pamoja na familia yangu". Amesisitiza Waziri Kombo akitolea mfano Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar namna linavyofana na kuwatangaza wasanii pamoja na kuwaongezea kipato.
Hata hivyo wanatasnia ya filamu mkoani Geita kwenye risala yao wamesema wanahitaji kupewa mafunzo zaidi juu ya namna ya kuboresha filamu zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi hizo hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao na kuahidi kufikisha mafunzo ya filamu mkoani Geita kama ilivyokuwa hivi karibuni mkoani Mwanza.
Post a Comment