Header Ads

Wadau wajadili Maombi ya Tanesco Kupandisha Bei ya Umeme

 Maimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Mhandisi Decklan Mhaiki, akiwasilisha mambi ya shirika hilo ya kupaandishi bei ya umeme kwa asilimia 18.9 wakati wa kikao cha majadiliano baina ya wadau na uongozi wa shirika, kilichoitishwa na Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), na kufanyika jijini Dar es Salaam, Novemba 23, 2016.

 Baadhi ya viongozi wa TANESCO na wadau wakifuatilia mjadala.




Na KHALFAN SAID

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wadau wa umeme kujadili maombi ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO ya kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.9 kwa uwazi na bila hofu lakini wakizingatia nia ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga nchi yenye uchumi wa viwanda.

Akifungua majadiliano ya wadau wa Mkoa wa Dar es Salaam, Zanzibar na uongozi wa TANESCO jijini Novemba 23, 2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Maji na Nishati, (EWURA), kuhusu mapendekezo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, (pichani juu), ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Paul Makodna alisema, “Rais wetu Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, amedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ambao utafanikiwa tu endapo tutakuwa na umeme wa uhakika na ulio bora.” Alisema.

Aliwataka wadau kusikiliza kwa makini hoja za TANESCO zinazowasukuma kupandisha bei ya umeme, lakini TANESCO nao wanapaswa kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo yao.

Akiwasilisha mapendekezo ya TANESCO kwa wadau, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Decklan Mhaiki, alisema, Shirika hilo limefikia uamuzi wa kuwasilisha mapendekezo hayo kulingana na mambo matatu ambayo ni kufua umeme (power generation), Kusambaza umeme (Power distribution), na kusafirisha umeme (Power transmission).

“Kama mjuavyo shirika limekuwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme kote nchini, kwa lengo la kuwapatia wananchi umeme ulio bora na wa uhakika, na kwakweli mabadiliko tayari yameanza kuonekana ambapo hivi sasa kadri siku zinavyokwenda mbele hali ya umeme wetu imekuwa bora zaidi.” Alisema Mhandisi Mhaiki.

Alisema, bei ya umeme hapa nchini ni ya chini ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Masharikiambapo alisema, wakati bei ya umeme kwa sasa, hapa Tanzania ni shilingi 242.21, wakati Kenya bei ni Shilingi za Kitanzania, 326 kwa unit, Uganda Shilingi 456 kwa unit, Rwanda Shilingi 438 kwa unit, na Burundi ni Shilingi 195 kwa unit.

“ Hata tukipandisha umeme bado Tanzania bei ya umeme itabaki kuwa chini ukilinganisha na majirani zetu ambapo, tunaomba unit moja ya umeme iuzwe kwa Shilingi 286.28, sawa na ongezeko la asilimia 18.9.” Alifafanua Mhandisi Mhaiki.

Akitoa hotuba ya ukaribisho, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), Felix Ngamlagosi, alisema, Mamlaka hiyo imepokea maombi ya TANESCO kupandisha umeme kwa mwaka mmoja kuanzia Januari hadi Desemba 2017, kama ambavyo sheria inavyotaka.

“Mamombi haya ya TANESCO ni halali yamekidhi sheria, na niwaombe wadau mtoe maoni ambayo yatasaidia pande zote mbili, TANESCO na watumiaji wa umeme, ili hatimaye wananchi waendelee kupata huduma bora ya umeme.” Alisema.

Mkurugenzi huyo alisema, tayari Mamlaka yake imekwisha kusanya maoni kutoka kanda wakilishi zote nchini nab ado wanakaribisha maoni zaidi yatumwe kwenye mamlaka yake hadi Novemba 25 mwaka huu saa 11 jioni ambapo dirisha la kupokea maoni litafungwa.

Kwa upande wa watoa maoni, Mwanasheria wa Shirika la Umeme Zanzibar, (ZECO), Abas Juma alsiema, kwa mujibu wa vigezo vilivyopelekea TANESCO kuomba bei ya umeme ipande, ni viwili tu ndio vinaihusu ZECO, ambavyo ni uzalishaji na usafirishaji umeme, na kwamba kazi ya kusambaza umeme inafanywa na ZECO yenyewe na kuliomba shirika la umeme TANESCO kuzingatia uhalisia huo na hivyo ZECO haistahili kulipa bei sawa nay a wateja wa TANESCO Tanzania bara.

Mwananchi mwingine ambaye ni mzalishaji umeme kwa kutumia bio-gas, ameipongeza TANESCO kwa kuboresha huduma zake na kuwataka wadau kulikubali ombi la Shirika hilo ili kuwezesha kasi ya uboreshaji huduma iweze kusonga mbele.

“Mimi ninaunga mkono maombi ya TANESCO, sisi wazalishaji umeme wadogo, tunashindwa kupata mikopo kutoka kwenye mabenki ya kuendesha miradi yetu maana mabenki hayana uhakika kama tunaweza kurejesha fedha zao kwa vile bei ndogo ya umeme inayotozwa na TANESCO hailingani na gharama za uendeshaji, hivyo wanahofia wasiweze kupata fedha zao.” Alisema.

Mwananchi mwingine ambaye ni Mfugaji aliipongeza TANESCO kwa kuboresha huduma za umeme na sasa hali ya umeme imeanza kuimarika. 

“Mimi ni mfugaji miaka miwili iliyopita nililazimika kununua taa za mchina, ili kuhudumia kuku wangu kwa vile umeme wa TANESCO ulikuwa hautabiriki, lakini hivi sasa zile taa sio muhimu tena kwangu kwani umeme unapatikana kwa uhakika lakini sio hivyo tu hata ubora wa umeme wenyewe umekuwa wa kuridhisha sana.” Alisema.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), Felix Ngamlagosi.

 Baadhi ya wajumbe wa bodi ya EWURA.

 Baadhi ya wadau na viongozi wa TANESCO.

 Baadhi ya wadau kutoka Zanzibar na viongozi wa EWURA.

No comments

Powered by Blogger.