Ziara ya PAUL MAKONDA : akatiza Vichochoro Kusaka Kero za Wananchi, KINONDONI
TUCHAPE KAZI KIONGOZI: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwaga kicheko na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mkoa huo, walipokuwa wkijadili jambo, baada ya kuzungumza na viongozi na watendaji kutoka wilaya ya Kinondoni, katika Bwalo na Maofisa wa Polisi, Msaki mwanzoni mwa ziara yake katika mkoa wa Dar es Salaam.
TANDALE................
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua chumba cha biashara cha Mamalishe (kushoto), aliyemkuta akiwa kazini eneo la Tandale, akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi.
Makonda akimwangalia mamalishe huyo wakati akiandaa chakula.
Makonda na msafara wake wakikatiza mitaa ya Tandale wakati akisaka kero za wananchi wakati wa ziara hiyo ya aina yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wanne ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
Salum Ali Hapi akimpa maelezo Makonda walipofika kukagua eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo Tandale, Kata ya Manzese.
SHULE...............
Makonda akitazama paa la chumba cha darasa katika shule ya Msingi Tandale, lililoporomoka wakati wa upepo mkali ulioambatana na mvua.
MIUNDOMBINU YA BARABARA.....................
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitazama majitaka yakitiririka kwenye daraja la barabara kutoka Tandale kwenda Mwananyamala. Makonda aliahidi barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami, la kwamba kabla ya hatua hiyo itafanyiwa matengenezo ya awali kuziba makorogoro ili iweze kupitika.
Makonda akipita pembeni pembeni kukwema maji machafu yaliyotuama kwenye sehemu ya barabara hiyo.
Mara huyu mama naye akamvaa na kumweleza kero zake wakati akipita.
MKUTANO UWANJA WA SHULE YA MSINGI TANDALE.........
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi akimkaribisha Makonda kuanza kuunguruma ili kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu papo hapo au baadae, katika mkutano wa hadhara uliofayika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Tandale.
Makonda akizungumza .
Makonda akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta.
Umati wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akifuatilia jambo kwenye simu yake wakati wa mkutano huo, Mpogolo ni miongoni mwa waratibu wa ziara hiyo ya siku kumi ya Makonda katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.
Wananchi kwenye mkutano huo....
Makonda akianza kujibu kero kwa kuwahoji watendaji kulingana na wananchi walivyotaka kujibiwa kero husika.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya (aliyeshika kinasa sauti), akisubiri hukumu ya Makonda baada ya kushindwa kueleza ikiwa alikuwa anajua au hajui kadhia ya dawa kuibwa mara kwa mara katika Zahanati ya Tandale kama wananchi walivyolalamika, ambapo alisema hajui.
" Haiwezekani uwe Mganga Mkuu wa Wilaya katika mkoa wangu halafu hujui kuhusu kuibwa kwa dawa kwenye zahanati, hii haikubaliki, kuanzia sasa si mganga Mkuu wa Kinondoni, Nitawaambia wizara inayokuhusu wakupangine wilaya katika mikoa mingine ambako watavumilia uzembe kama papo", alisema Makonda wakati akimtumbua Msuya kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika shule ya Msingi Tandale.
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Post a Comment