Rais wa Rotary club ya Oster bay akizungmza na waandishi wa habari kuhusu utoaji Huduma ya bure ya Afya kwa wakazi wa kerege Bagamoyo siku ya jumapili ya tarehe 27 mwezi Huu.
..........................................................
Klabu ya Rotary ya Oyster Bay imeandaa kambi
ya matibabu ya bure itakayofanyika eneo la Kerege wilayani Bagamoyo.
Huduma
hizo za matibabu zitatolewa siku ya Jumapili tarehe 27 Novemba katika shule ya
Msingi ya Kerege.
Timu ya
wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali, wanafunzi wa udaktari, wanachama
wa Rotary na wafanyakazi wa kujitolea kutoka sekta mbalimbali watashiriki
katika kambi hiyo ya matibabu.
Vipimo na
matibabu yatatolewa kwa magonjwa kama malaria, upungufu wa damu, kisukari na
shinikizo la damu, masikio, pua na koo (ENT), magonjwa ya ngozi, macho, meno na
kansa ya kizazi kwa akina mama.
Miwani zitatolewa kwa watu watakaokutwa na
matatizo ya macho.
Huduma za ushauri kwa wajawazito zitatolewa na wajawazito
pia watapatiwa vifaa vya kujifungulia bure.
Wakazi wa Kerege
na maeneo ya jirani wanaombwa kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo ya
matibabu ya bure haswa akina mama na watoto.
Akizungumza
kuhusu mradi huu, Alfred Woiso, Rais wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay alisema,
“Tuna furaha kuandaa kambi hii kwa mara nyingine tena kwa wakazi wa Kerege
ambapo lengo letu ni kuwasaidia watu ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za
matibabu.
Tunawashukuru wadhamini na watu wote wanaojitolea katika mradi huu na
tunakaribisha watu kuhudhuria na kusaidia kwa namna yoyote ile katika kambi hii
ya matibabu.”
Usajili wa
matibabu utaanza mapema asubuhi na watu wapatao 1,200 wanatarajiwa kupata
huduma za matibabu kulingana na mwenendo wa idadi ya watu ambao huwa
wanajitokeza kila mwaka kambi hiyo inapofanyika. Wakazi wa Kerege wanashauriwa
kufika mapema ili kuweza kupata huduma.
Kambi hiyo ya matibabu imedhaminiwa na Diamond
Trust Bank na inaandaliwa kwa ushirikiano na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital
Supplies, Whitedent, vClick Concepts Inc, MAK Books and Brains, ABACUS
Pharmaceuticals, Fazel Foundation na wanachama wa Klabu ya Rotary na Rotaractor.
Kambi
ya kwanza ya Matibabu kuandaliwa na Klabu Ya Rotary ya Oyster Bay ilifanyika Chanika
mwaka 2011 na zaidi ya watu 600 walipimwa
malaria, UKIMWI, kisukari, Masikio, Pua na Koo, Macho na magonjwa mengine sugu.
Dawa pamoja na miwani zilitolewa bure kwa watu waliokutwa na matatizo. Mwaka 2012
watu zaidi ya 700 walipatiwa matibabu, sawa na mwaka 2013 na 2014.
Mwaka 2015
idadi ya watu waliopata huduma ilipanda hadi kufikia zaidi ya watu 1,200. Mwaka
huu pia idadi hiyo ya watu 1,200 inatarajiwa kupata matibabu.
|
Post a Comment