Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemavu lafanyika Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi, akizungumza wakati akizindua tamasha la tano ya watu wenye ulemavu nchini, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa kwa udhamini wa Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation of Civil Society.
******************************
Naibu
Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu
wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi leo amezindua tamasha la tano ya
watu wenye ulemavu nchini, Tamasha lililoandaliwa kwa udhamini wa
Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation of Civil Society,
lililofanyika katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
Dk.
Posi amebainisha katika Tamasha hilo kuwa, serikali ipo karibu na
watu wenye ulemavu na kwamba sheria iliyopitishwa mwaka 2010, kuhusu
watu wenye ulemavu imepitishwa na kwamba ni jukumu la jamii nzima
kushirikiana katka kutoa haki sawa kwa wananchi wote wakiwemo
walemavu.
Dk.
Posi alifafanua kuwa, changamoto zinazowakabili walemavu hapa nchini
ni nyingi lakini pia serikali inazitambua, inazichambua na
inazifanyia kazi kwa kadri uwezo unapopatikana.
Kabla
ya hotuba ya Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for
Civil Society, Fransis Kiwanga alifafanua kuwa, shirika analoliongoza
kwa kutambua umuhimu wa kuwawezesha walemavu hapa nchini, liliona ni
busara kuchangia kuwepo kwa tamasha hili na kwamba ni faraja kwa
shirika hili kuona maisha na hali ya walemavu hapa nchini
inabadilika.
Mkurugenzi huyo alisema na kuongeza kuwa, shirika lake kwa kutambua
haki mbalimbali za walemavu na hali halisi ya maisha hapa nchini,
linaiomba serikali kuhakikisha kuwa inakuwa karibu na watu wenye
mahitaji maalum ili nao wajione kuwa ni raia wa daraja la kwanza
katika nchi yetu.
Tamasha
hili linalounganisha wawakilishi wa watu wenye mahitaji maalum kutoka
pane zote za Tanzania, linafanyika kwa siku mbili na likihusisha
wawakilishi wapatao 150 kutoka katika mikoa yote nchini Tanzania na
linafanyika hapa jijini Dar es Salaam kwa siku mbili.
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo.
Mshiriki Kaganzi Rutachwamagyo, akichangia mada.
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo.
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Shiriki lisilo la Kiserikali la Foundation for Civil Society, Francis Kiwanga, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Tamasha hilo kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam,leo.
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo.
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo.
Makamu Mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Ummy Nderiananga akisoma Risala kwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo.
Post a Comment