TRA yatoa Elimu ya Mlipakodi Kwa Wafanyabiashara Raia wa CHINA
Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA Bi. Diana Masalla akitoa elimu ya mlipa kodi na sheria za kodi kwa wafanyabiashara raia wa China wanaoishi hapa nchini na kufanya biashara katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam, ambapo kabla semina hiyo imefunguliwa na Bw. Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibiashara kutoka serikali ya Watu wa China nchini Tanzania, Semina hiyo inalenga kuwapa wafanyabiashara hao elimu na uelewa wa masuala mbalimbali ya kisheria katika kodi na umuhimu wa kulipa kodi.
Baadhi ya wafanyabiashara raia wa China wanaoishi nchini Tanzania na kufanya biashara wakiwa katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam.
Post a Comment