Rais wa Wachimba Madini Ajitosa Kumsaidia Dkt JOHN MAGUFULI
Rais wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania (FEMATA ) Bw John Bina akitambulishwa mbele ya balozi wa China nchini (hayupo pichani) kulia ni waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba.
Bw John Bina akihamasisha uchangiaji wa madawati mashuleni.
balozi wa Chini Nchini Tanzania Dr Lu Yonq.ng katikati akiwa na viongozi wa mkoa wa Shingida kutoka kulia mkuu wa mkoa wa Singida Bw Methew Mtigumwe,waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ,mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Bi Martha Mlata na Rais wa FEMATA Bw John Bina.
Na Francis Godwin
RAIS wa shirikisho la vyama
vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) ametoa
wito kwa wachimbaji wote yakiwemo
makampuni makubwa ya uchimbaji wa
madini kujitokeza kumuunga mkono Rais Dr John Magufuli katika harambee ya kuchangia madawati kwa
shule mbali mbali hapa nchini.
Huku akisifu mwitikio mzuri wa kampuni ya Sunshine Minning kwa
kuunga kuitikia wito huo kwa kuchangia madawati 100 yenye thamani ya Tsh
milioni 85,000 kwa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida .
Akizungumza na waandishi
wa habari jana ,Rais wa FEMATA John Bina alisema kuwa Shirikisho lake
limelazimika kumsaidia Rais Dr
Magufuli kuhamasisha uchangiaji wa madawati
kwa wanachama wake ili kumaliza kabisa tatizo hilo la uhaba
wa madawati na kuona sekta ya elimu nchini inaboresheka
zaidi kwa
kuhakikisha wanafunzi hawakai chini.
Bw Bina alisema kuwa
katika kuunga mkono jitihada za serikali wao kama sehemu
ya wadau wa maendeleo katika Taifa hawakupenda kuwa nyuma
kujitokeza kuchangia madawati hasa ukizingatia kuwa
elimu bora ni mwanzo wa kuwa na taifa bora .
"Suala hili la
elimu si la serikali pekee kila mmoja kwa nafasi yake ana umuhimu katika
kuboresha elimu nchini na si vema kwa
kila jambo kuitazama serikali ......serikali ina
nafasi yake ila na sisi wadau tuna nafasi yetu
katika kuiunga mkono serikali pia wanafunzi wananafasi yao
.... walimu na wazazi pia " alisema rais Bina
Hata hivyo
aliwataka wadau wengine na wananchi
mmoja mmoja kwa nafasi yake kujitokeza kuunga mkono uchangiaji wa
madawati ili kumaliza kabisa kero hiyo ya uhaba wa madawati
mashuleni.
Alisema wao kama wadau
wa maendeleo kupitia FEMATA wataendelea kuunga mkono
jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na serikali ya
Rais Dr Magufuli jitihada zenye lengo la kulifanya
Taifa kuzidi kuwa mbele kimaendeleo.
Pia
alisema kwa wadau wa
sekta hiyo ya madini pekee
kama kila mmoja atajitolea kuchangia madawati upo
uwezekano mkubwa wa zoezi hilo kukamilika mapema zaidi na kuwataka wadau
wengine mbali ya wale wa
madini nao kwa nafasi zao
kujitolea madawati badala ya kuiachia
serikali pekee.
“ Ninakusudia kama
Rais wa FEMATA kuwakutanisha
wachimbaji wote mbali na mambo
mengine tutaangalia ushiriki
wetu katika masuala ya kijamii
yakiwemo ya uchangiaji wa madawati”
Hata hivyo mkuu
wa mkoa wa
Singida Bw Methew Mtigumwe mbali ya
kupongeza harakati za Rais huyo wa FEMATA kwa
kuunga mkono agizo la rais kwa
kujitolea kuhamasisha uchangiaji
wa madawati bado alisema
kuwa jambo hilo ni jema na linapaswa kupongezwa zaidi.
Alisema katika mkoa wa Singida
kila mkuu wa wilaya
ameagizwa kusimamia utekelezaji wa agizo
la Rais la upungufu wa madawati katika eneo lake na kuwa mkoa umejipanga kumaliza kabisa kero
hiyo ya uhaba wa madawati .
Post a Comment