Header Ads

Jinsi TIGO MUSIC inavyobadili Maisha ya Wanamuziki wa Kitanzania


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MUZIKI wa kizazi kipya maarufu kama ‘Bongo Flava’ ulikuwa haujulikani na pia haukuonekana kama ni sanaa halisi ya muziki;  hivi ndivyo ambavyo vizazi vilivyotanguliwa vlivyoutazama takribani miongo miwili iliyopita japo ni muziki wa kuburudisha watu wa rika zote wadogo kwa wakubwa.

Muziki wa ‘Bongo Flava’ umebadilisha himaya ya muziki hapa Tanzania ambao umepata sifa  katika nchi za Afrika mashariki, Afrika na Ulaya.

Ni ukweli usiofichika kuwa, sekta ya muziki wa kizazi kipya imekuwa kwa kasi na hata kuwapatia ajira vijana wengi wa kitanzania wenye vipaji ambao walikuwa hawana kazi hapa nchini kufuatia tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto kwa vijana.

Ingawaje fani ya muziki imwekuwa ikionekana kuwa na maendeleo yanayosuasua kwa kipindi cha muongo mmoja hivi, wasanii wa muziki bado wanakumbana na changamoto nyingi.

Wameeleza changamoto hizo kuwa ni mapungufu ya kuwezeshwa kitaifa na kimataifa na kuwepo kwa ujuzi mdogo miongoni mwa wanamuziki.

Kuna baadhi ya makampuni, mashirika na hata watu binafsi ambao wameona umuhimu wa kutatua matatizo kama haya yanayowakabili wasanii na wanamuziki hapa nchini, na badala yake wamegundua mikakati ya kuwawezesha ili kutimiza malengo na ndoto zao kwa ujumla.

Tigo Tanzania ni moja ya makampuni hayo, na kwa kuwa ni kampuni ya kidijitali inayobadili maisha ya watumiaji mtandao wake, kampuni hii ilianzisha jukwaa la wanamuziki wa kizazi kipya ijilikanayo kama ‘Tigo Music Platform’  ambayo inalengo la kuwawezesha wasanii wa muziki hapa nchini na kufanya kazi zao zijulikane ndani na nje ya nchi.

Hadi sasa Tigo imekwisha wawezesha wanamuziki wa kitanzania wapatao 20 kupitia program yake ya Tigo Music Platform tangu ilipoanzishwa mnamo mwezi Januari 2015.

Wakiongea katika nyakati tofauti, baadhi ya wanamuziki ambao wamefaidika na  program ya Tigo Music walisema kuwa kupitia jukwaa hilo, miziki ya watanzania na wasanii wa muziki wamejulikana kimataifa.

Hii ni kwa sababu kuwa washabiki wa muziki hasa wa kizazi kipya kutoka kila kona hapa duniani wamekuwa wakipata miziki hii kupitia mfumo wa kusambaza miziki hiyo kwa njia ya mtandao wa kimataifa ujulikanao kama ‘streaming’.

“Kwa kupitia mtandao huu, wasanii wa muziki wa kitanzania wamepata fursa ya kujulikana kimataifa, na vile vile kuweza kupata fedha za ziada kutokana na mmiziki yao, na hii ndiyo ilikuwa lengo kuu la kuanzisha mtandao huu unaowaunganisha na washabiki wa miziki hiyo”, alisema mawanamuziki nguli wa Bongo Flava mwenye asili ya Kongo, Christian Bella katika mahojiaono maalumu mwaka jana. 

Taarifa kutoka Tigo inasema kuwa, program ya Tigo Music pia inatoa mafunzo kwa wanamuziki ili kuwajengea uwezo wasanii wa muziki hasa wa kizazi kipya wanaoibukia ili wajue ualisia wa mali zao kama muziki kuwa ni mali na masoko pia ili waongeze ujuzi wao na kujenga maisha yao kuwa bora.

“Mtandao wa kusambaza miziki duniani kote unakuwa kwa haraka, na vilevile ni wa pili kujilikana kama mtandao wa simu kusini mwa bara la Afrika”, inasema taarifa hiyo na kuongeza kuwa huu ni mtandao wa kidijitali kwa ajili ya maisha ya kisasa ambao Tigo imeutumia kuwezesha ukuaji wa vipaji vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

Inaendelea kusema kuwa Tigo imekuwa ikiwatia moyo wanamuziki wa ndani kuwa karibu na shirika la haki za muziki barani Afrika, yaani ‘Africa Music Rights’ ambao huwadhamini na kupandisha chati haki za muziki barani Afrika ili wanamuziki waweze kutawala soko la muziki hapa Afrika.

Kwa sasa Tigo Tanzania imekuwa karibu sana na kampuni ya kimataifa ya kifaransa ambayo kazi yake kubwa ni kusambaza miziki duniani ijulikanayo kama ‘Music Streamer Deezer’.

Kampuni hii hutoa huduma zake kwa ajili ya kusambaza na kupata miziki zaidi kote duniani kupitia simu za mkononi, ambapo inatoa njia 36 milioni za kutapa miziki mbalimbali duniani.

 Akizungumzia mtandao wa muziki wa Tigo yaani ‘Tigo Music’ wakati akihojiwa jijini Dar es Salaam, mwanamuziki wa kizazi kipya wa muziki wa ‘Bongo Flava’ ambaye ni mmoja wa wanaofaidika na mtandao huu, David Genz maarufu kama ‘Yangdee’ alisema kuwa program ya muziki wa Tigo Music imemuwezesha kujulikana katika nyanja ya kitaifa na kimataifa.

Yangdee aliongeza na kusema: “kuanzishwa kwa program ya ‘Tigo Music Platform’ ni ukombozi kwa wanamuziki wachanga wanauibukia hapa nchini kwa kuwa imetuwezesha kujulikana kimataifa, tunaishuukuru kampuni ya Tigo Tanzania kwa kutusaidia”.

Alikuwa akiongea wakati alipokuwa na wenzake ambao pia wanaonufaika na mpango huu wa Tigo Music wakati walipotembelea moja ya maduka ya Tigo yaliyopo jijini Dar es Salaam katika ziara maalumu iliyolenga kubadilishana mawazo kuhusu kazi zao za muziki.

 Christian Bella naye anaongeza kuwa anaishukuru Tigo kwa ubunifu wake hasa pale ilipoanzisha program hii ya Tigo Music ya kuwawezesha wanamuziki wa kitanzania.

 Katika mahojiano yake na waandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za Tigo makao makuu, Bella alisema: “ninayo heshima kubwa kuisifu Tigo kwa kuwa imepandisha chati miziki ya wasanii hapa Tanzania”. 

Ni matumaini yangu kuwa msaada wa Tigo utaendelea kuwasaidia wanamuziki wa Tanzania katika kukuza fani ya muziki nchini”.

Tigo Music ilizinduliwa hapa Tanzania mwezi Januari 2015 ambapo Meneja wa Nembo wa Tigo, Bw. William Mpinga alisema kuwa ina lengo la kukuza kazi za wanamuziki na kuendeleza ukuaji wa soko la wanamuziki wa ndani.

No comments

Powered by Blogger.